Habari za Punde

Maradhi Yasiyoambukiza Zanzibar

Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja wa Kitengo cha Maradhi Yasiyoambukiza kutoka  Wizara ya Afya Zanzibar Omar Abdalla Ali  (hayupo pichani ) ihuko katika Ofisi ya Jumuiya ya maradhi  Yasiyoambukiza,, Mpendae.
Meneja wa Kitengo cha Maradhi Yasiyoambukiza kutoka  Wizara ya Afya Zanzibar Omar Abdalla Ali  akitoa ufafanuzi juu ya ongezeko la maradhi yasiyoambukiza Zanzibar ambalo limeonyesha kusababisha vifo vya watu weng,ihuko katika Jumuiya ya maradhi  Yasiyoambukiza, Mpendae. 


 Na Khadija Khamis- Maelezo Zanzibar    08/11/2020.

Meneja wa Kitengo cha Maradhi yasiyoambukiza Zanzibar Omar Abdalla Ali amesema maradhi yasiyoambukiza yameongoza kupoteza maisha ya watu wengi duniani wa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2016 hadi 2018.

 Akizungumza na waadishi wa habari ofisini kwake Mpendae Zanzibar alisema tafiti  zilizofanywa zimeonesha  kuwa maradhi ya shindikizo la damu na kisukari yameongoza kupoteza maisha ya watu wengi kila mwaka  kwa mujibu wa taarifa za Wizara ya Afya Zanzibar  .

Alisema taarifa zimeonesha kuwa Wizara ya Afya inaongoza kupokea wagonjwa wa maradhi yasioambukiza na kati yao wagonjwa wanaougua, wanaolazwa lakini wanaopoteza maisha ni wagonjwa sita katika kila wagonjwa kumi wanaofika vituo vya afya kwa matibabu.

Amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa katika hospitali kuu ya mnazimmoja  ambao pia kupoteza maisha kwa maradhi hayo ukiwemo ugonjwa wa shindikizo la damu ,kisukari, saratani ya kensa ya titi,kensa ya shingo ya kizazi, kensa ya tenzi dume, ajali za barabarani, ugonjwa wa akili,pamoja na maradhi yanayosababishwa kwa njia ya hewa ikiwemo pumu  .

“Maradhi haya sio Zanzibar tu bali duniani kote kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la maradhi yasioambukiza ikiongoza shindikizo la damu” alisema Meneja Omar

Alifahamisha kuwa ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa muda mrefu unaotokana na ongezeko la sukari mwilini, isiyokuwa ya kawaida ambayo huonekana katika kipimo cha sukari katika damu wakati mtu anapopimwa kabla ya kula na baada ya kula.

Nae Meneja wa Jumuiya ya Maradhi Yasioambukuiza Zanzibar Haji Khamis Fundi amewataka wanajamii wajenge utamaduni wa kula chakula bora zikiwemo mbogamboga ili kuweza kuupa mwili afya njema na kuongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

  “Haikatazwi kula vyakula vya uwanga lakini tutumie mchanganyiko wa vyakula ikiwemo matunda na mbogamboga na samaki epukeni matumizi ya soda tamu pipi chakleti na biskuti tumbaku na pombe” alisema Meneja huyo.

 Aidha aliwashauri wanajamii kujiwekea utaratibu wa kupima afya na kufanya mazoezi kwa dakika isiyopungua 30 kwa kila siku ili kuufanya mzunguko wa damu kuweza kufanyakazi vizuri na kuuweka mwili katika hali ya wastani unaotakiwa.

Hata hivyo aliwataka wauguzi kutoa ushirikiano mzuri kwa wananchi wanapohitaji huduma ikiwemo vipimo katika vituo mbali mbali  vya afya ili kuweza kuwapatia matibabu mazuri na kwa haraka .

Maadhimisho ya siku ya Kisukari duniani hufanyika Kila ifikapo Novembar 14 kila mwaka.           

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.