Jaji Mkuu Wa Zanzibar, Omar Othman Makungu akiwasilisha mada inayohusu uhusiano wa Baraza la Wawakilishi na mihimili mengine katika mafunzo elekezi kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi yanayofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani
Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe, Omar Othman Makungu amesema kuna umuhimu mkubwa wa mihimili mitatu ya dola kushirikiana katika utendaji wa kazi zao ili kuweza kuwahudumia vizuri wananchi katika kuwaletea maendeleo.
Jaji Othman makungu ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada ya “uhusiano wa Baraza La Wawakilishi na mihimili mengine” katika mafunzo elekezi kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi yanayoendelea katika ukumbi wa Baraza hilo Chukwani.
Amesema lengo kubwa la vyombo hivyo ni kugawana madaraka katika kutoa huduma bora kwa wananchi katika misingi ya demokrasia ambapo malengo hayo hayatofikiwa ikiwa vyombo hivyo vitakua na migogoro ndani yake.
Amefahamisha kuwa kwa upande wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla vyombo hivyo vitatu vinafanya kazi kwa mashirikiano makubwa ambayo yameipelekea serikali kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi wake.
Wakati huo huo balozi mstaafu Dkt Mahadhi Juma Maalim akiwasilisha mada inayhusu “mgawanyo wa madaraka na kazi za Baraza la wawakilishi” amewasisitiza wajumbe wa baraza hilo kujifunza kwa umakini sheria na kanuni zinazoongoza utendaji wa kazi wa baraza pamoja na kuwatumia wataalamu wa baraza hilo kuweza kutekeleza majukumu yao kwa uweledi mkubwa.
No comments:
Post a Comment