Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali aanza kazi akagua maendeleo ya ukarabati wa Skuli ya Benbella

          
Mkandarasi kutoka kampuni ya Modern Building Constructions, Bwana Ali Pandu Shara akimpa maelezo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohamed Said wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ukarabati wa Skuli ya Sekondari Ben bella Mkoa wa mjini magharibi Unguja.Skuli kongwe ya BenBella ambayo sasa inafanyiwa ukarabati mkubwa
         
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohamed Said (wa kwanza kushoto)akipokea maelezo kutoka kwa mkandarasi (wa kwanza kulia) kutoka kampuni ya Modern Building Constructions Bwana Ali Pandu Shara wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ukarabati wa Skuli ya Sekondari Ben bella Mkoa wa mjini magharibi Unguja.

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amewataka Wakandarasi waliokabidhiwa kufanya ukarabati wa Skuli ya Sekondari Benbella kuhakikisha wanamaliza kazi kwa wakati na katika kiwango bora.
Amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ukarabati wa Skuli hiyo, amesema yale malipo wanayopatiwa ni vyema kuhakikisha kuwa yanaendana na kasi ya kazi yao.
Aidha amewaagiza wahasibu na waangalizi wa hesabu za ndani wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhakikisha malipo yanayofanyika kupitia matengenezo ya Skuli hiyo kuwa yanaendana na kazi itakayofanyika tena kwa usahihi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Modern Building Constructions Bwana Ali Pandu Shara, ameiahidi Wizara ya Elimu kuwa watafanya kazi kwa kiwango bora zaidi kwani wanaamini fedha itakayolipwa kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa Skuli hiyo inatokana na kodi za wananchi hivyo ni busara kuzitendea haki fedha hizo kwa kukamilisha ujenzi kwa wakati na kiwango bora.
Wakati huo huo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amefanya ziara katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Kiswahili na lugha za kigeni SUZA uliipo Vuga mjini Unguja na kuangalia maeneo yaliozunguka na kuutaka uongozi wa Skuli hiyo kuufanyia ukarabati sehemu hizo kutokana na fedha zinazofanyiwa malipo kwani upo katika hali isiyoridhisha .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.