Habari za Punde

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale aunda kamati kuchunguza fedha zilizopotea sekta ya utalii

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Lela Muhammed Mussa (katikati ) akitoa tathmini  ya ziara yake ya wiki moja kwa Waandishi wa habari huko katika Ukumbi wa Wizara Kikwajuni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utalii  na Mambo ya Kale Bi Khadija  Bakar akifungua Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Viongozi wa Wizara katika Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo huko katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Lela Muhammed Mussa akitoa tathmini  ya ziara yake ya wiki moja kwa Waandishi wa habari huko katika Ukumbi wa Wizara kwake Kikwajuni.

NA KHADIJA KHAMIS- MAELEZO ZANZIBAR

Mwashungi Tahir -  Maelezo      30-11-2020

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Lela Muhamed  Mussa  amesema ameunda kamati ya watu watano ili kuchunguza fedha zilizopotea kutokana na mianya unaotumika ambayo sio sahihi ndani ya sekta ya utalii.

Ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Utalii na mambo ya Kale  ulioko Kikwajuni wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojitokeza kwenye ziara yake na kuibua changamoto ikiwemo mambo matatu ambayo yaliyojitokeza hapa Unguja.

Amesema kamati hiyo itawahusisha  sekta zote za Wizara hiyo ikiwemo mtaalamu wa mji Mkongwe,Utalii na mambo ya kale, Mwasheria na wengineo  kwa ajili ya kujua undani wa miradi yote ya ndani wizara hiyoambayo  hakuweza kuridhika nayo.

Hata hivyo amesema lengo la  kamati hiyo ni kufanya upembuzi yakinifu ya miradi yote ambayo inatarajiwa kuchukuwa wiki moja kukamilika kwake .

Pia amesema hakuridhishwa na  ufinyu wa majengo ya wafanyakazi ikiwemo Wizara, Kamisheni na kuamua kujengwa Majengo ya nafasi ili kuondosha changamoto kwa wafanyakazi hao  .

Aidha amesema hajaridhishwa na malimbikizo ya madeni kwa wafanyakazi ikiwemo muda wa ziada, maposho yao pamoja na walinzi kutopata stahiki zao kwa muda mrefu na ukosefu wa usafiri, jambo ambalo linazorotesha ufanisi wa kazi .

“sijaridhishwa na malimbikizo ya madeni kwa wafanyakazi jambo hili linachangia kutokuwa na ufanisi kwa watendaji kwani wanavunjika moyo kutowalipa haki zao “alisema Waziri huyo.

Vile vile amesema kwa upande wa Utalii kuna upotevu mkubwa wa mapato na kufatilia jambo hili ili mapato yaweze kupatikana  itabidi kutumika mfumo wa elektronik  ambao mfumo huo utaweza kuziba mianya na kuepuka upotevu ulioko hivi sasa.

“Mapato yote yataweza kufanywa kwa mfumo wa electronic ili yaweze kuingia kwa pamoja na kuweza kudhibiti mapato ya Serikali katika sekta ya Utalii,” alisema Waziri Lela.

Hivyo alisema katika ziara hiyo aliweza kuona uvamizi uliojitokeza katika  maeneo ya nyumba za kihistoria .

Amesema kuhusu ujio wa utalii nchini watalii wameanza kuja kwa wingi baada ya kumalizika kwa janga la  Corona  imekuwa ni chachu kwa kuhamasisha utalii na kukuza pato la serikali

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.