Na JaalaMakame Haji - ZEC
Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar ZEC imewatangaza wajumbe kumi na nane 18 kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa
nafasi za Viti Maalum vya Wanawake vya Ujumbe wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar.
Tume imetangaza majina ya
Wajumbe hao katika Mkutano wake uliofanyika leo 07/11/2020 katika ukumbi wa mikutano
wa Tume hiyo Maisara Jijini Zanzibar.
Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar imewatangaza wajumbe 18 kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa mujibu wa masharti
na maelekezo ya Ibara ya 67 ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.
Aidha Tume imewatangaza
wajumbe hao baada ya kuridhika kuwa wote wana sifa ya kuwa Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar kama zilivyoainisha katika Katiba ya Zanzibar Ibara ya 68.
Waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ni
1.Bi.Panya Ali Abdallah.
2 Bi. Bihindi Hamad Hassan.
3.Bi.Salma Mussa Bilal.,
4.Bi.Shadya Mohammed Suleiman.
5, Bi.Fatma Ramadhan Mohamed (Mandoba).
6. Bi.Saada Ramadhan Mwenda.
7. Bi.Mwantatu Mbaraka Khamis.
8.Bi.Zainab Abdalla Salum.
9. Bi.Riziki Pemba Juma.
10. Bi.Leila Mohamed Mussa.
11. Bi.Salha Mwinyi Juma.
12. Bi.Hudhaima Mbarak Tahir.
13. Bi.Sabiha Fil fil Thani.
14. Bi.Aza Januar Joseph.
15. Bi.Mwanaid Kassim Mussa.
16. Bi.Mgeni Hassan Juma.
17. Bi.Mwanajuma Kassim Makame.
18. Bi.Rahma Kassim Ali.
Tume tayari imeshawasilisha
Majina ya Wajumbe hao kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa ajili ya
Hatua nyengine za Kisheria.
No comments:
Post a Comment