Habari za Punde

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali kugawa Mabuku ya Wanafunzi kwa Skuli zote Unguja na Pemba

Hii ni sehemu ya mabuku ya wanafunzi ambayo imenza kugawiwa leo kwa baadhi ya Walimu Wakuu skuli mbalimbali za Unguja waliofika katika Skuli ya Sekondari ya Dr Salmin Amour Juma iliyopo Chumbuni mjini Unguja kwa ajili ya kukabidhiwa mabuku ya wanafunzi na ya mahudhurio 


Baadhi ya Walimu Wakuu wa skuli mbalimbali za Unguja waliofika katika Skuli ya Sekondari ya Dr Salmin Amour Juma iliyopo Chumbuni mjini Unguja kwa ajili ya kukabidhiwa mabuku ya wanafunzi na ya mahudhurio
MKURUGENZI Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, bi Asya Idi Issa akiwagawia mabuku ya Wanafunzi na pamoja na mabuku ya mahudhurio, walimu wakuu wa Skuli mbalimbali za Unguja iliyofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Dr Salmin Amour Juma iliyopo Chumbuni mjini Unguja.
MKURUGENZI Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, bi Asya Idi Issa akiwagawia mabuku ya Wanafunzi na pamoja na mabuku ya mahudhurio, walimu wakuu wa Skuli mbalimbali za Unguja iliyofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Dr Salmin Amour Juma iliyopo Chumbuni mjini Unguja.
 
MKURUGENZI Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, bi Asya Idi Issa akizungumza na baadhi ya , walimu wakuu wa Skuli mbalimbali za Unguja baada ya kuwagawiwa mabuku ya wanafunzi na ya mahudhurio katika Skuli ya Sekondari ya Dr Salmin Amour Juma iliyopo Chumbuni mjini Unguja.
 

Na Maulidi Yussuf, WEMA

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inaendelea kutekeleza Sera ya Elimu Bila ya Malipo kwa kugawa Mabuku ya Wanafunzi kwa Skuli zote Unguja na Pemba.
Akizungumza wakati alipokabidhi mabuku hayo kwa Walimu wakuu wa Skuli mbalimbali za Sekondari za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Unguja, katika viwanja vya Skuli ya Dr Salmin Amour Juma iliopo Chumbuni Unguja, Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Bi Asya Iddi Issa amesema mabuku hayo ni ya aina mbili yenye karatasi 400 na mengine yenye karatasi 200.
Aidha Bi Asya amefahamisha kuwa mgao wa mabuku hayo utatolewa kwa elimu ya lazima ya Sekondari ambayo kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne ambapo amesisitiza kuwa mabuku mapya zaidi watapatiwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kutokana na kuwa ndio wanaoanza Sekondari.
Pia amesema kwa upande wa Wanafunzi wa kidato cha tatu na channe wao hawatopatiwa mabuku mapya kila mwaka na badala yake watapewa mpaka pale mwanafunzi buku lake litakapojaa.
Sambamba na hayo Bi Asya amesema, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imetoa dokezi maalum linaloonesha muongozo mzima wa ugawaji pamoja na matumizi ya mabuku hayo ikiwa lengo ni kuwapatia Wanafunzi ili waweze kuandikia wakiwa Skuli, kufanya kazi za nyumbani na kupitia yale waliyoyaandika.
Amesema kuna malalamiko juu ya mtumizi mabaya ya mabuku yaliyoanza kutolewa kwa Skuli za Maandalizi na Msingi kwa kutumika kinyume na lengo lililokusudiwa ikiwemo kutumika hospitali na wengine wasiokusudiwa.
Hata hivyo Bi Asya ameitaka jamii na Wanafunzi kwa ujumla, kuwa na utamaduni wa kutunza rasilimali zao ikiwemi vifaa vya Serikali kwani imekuwa ikitumia gharama kubwa kununua bidhaa mbalimbali kwa kuwafikikishia wananchi ikiwemo mabuku ili kuwapunguzia mzigo wanafunzi, ikiwa lengo ni kuleta maendeleo katika nchi.
Nae mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari Dr Salmin Amour Juma mwalimu Ramadhan Hassan Juma ameipongeza Serikali ya awamu ya 8 kwa kuanza vyema uongozi wake pamoja na kuipongeza Serikali iliyo pita chini ya uongozi wa Dk Ali Mohamedi Shein kwa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo Sera ya Elimu Bila ya malipo kwa kutoa vifaaa mbali mbali bure yakiwemo mabuku.
Jumla ya mabuku laki tatu na thalathini na saba elfu na kumi na nane yametolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Skuli zote za Sekondari za Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.