Habari za Punde

Kiongozi wa ACT Wazalendo akutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wateule wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama Cha ACT-Wazalendo


 Leo tarehe 1701/2020. Kiongozi wa Chama (KC) Ndugu Zitto Zubeir Kabwe amekutana na kufanya Mazungumzo na Wajumbe wateule wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama Cha ACT-Wazalendo

Pamoja na mambo mengine amewataka Wajumbe hao kufanya kazi kwa bidii, mashirikiano na weledi katika kuwatumikia Wananchi wa Zanzibar.
Kiongozi wa Chama aliwasisitiza nidhamu na Uwajibikaji ndio msingi muhimu Sana katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kikao hicho kilihudhuriwa kwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Ndugu Nassor Ahmed Mazrui, na Mwanasheria Mkuu wa Chama Ndugu Omar Siad Shaaban ambao wote kwa pamoja Ni Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Uteuzi wa Rais wa Zanzibar, pia Katibu wa Idara ya Bunge, Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa Ndugu Hamad Mussa Yussuf alimshukuru Kiongozi wa Chama kwa kuja kukutana na kuwapa maelekezo na mwongozo Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, ameahidi maagizo yote yaliyopokea yatafanyiwa kazi na kwa mashirikiano na Wawakilishi wataweza kuwahudumia Wananchi na Chama kwa ujumla.
Kikao hicho kimefanyika wakati Wawakilishi hao Wateule wakijiandaa kushiriki kwenye Vikao vya Baraza la Wawakilishi hapo February 10, 2021. Katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi hapo Chukwani, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Hamad M.Yussuf
Katibu wa Bunge, Baraza la Wawakilishi na serikalini za mitaa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.