Chama Cha waandishi wa habari
wanawake Tanzania, Zanzibar, (TAMWA ZNZ) tunapenda kumpongeza Mkurugenzi wetu Dr. Mzuri Issa kwa kupata tunzo ya kutoa mchango mkubwa katika jamii kwenye
maisha yake. Tunzo hizo zimeolewa na waandaaji wa Tunzo za Vijana Zanzibar
(ZYA) hii ikiwa ni mara ya pili mfululizo.
Mkuu wa jopo la majaji Bw Rashid
Mohammed Rashid, alisema mara hii pamoja na kuitoa zawadi kwa vijana wameona
pia watowe tunzo kwa watu waliosaidia sana maendeleo ya vijana nchini.
Wengine wanne walipewa tunzo hizo ni
Daudi Kombo Maalim, Shaib Ibrahim Mohamed, Raza Lee na DJ Saleh katika ghafla
iliyohudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana Mh Tabia Mwita huko Michenzani Mall
jana usiku.
Dr. Mzuri amepata tunzo hiyo kutokana na
kuwawezesha vijana wanawake katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment