Na Miza Kona Maelezo/ Zanzibar 18/01/2021
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema Zanzibar ni nchi yenye historia ya amani hivyo ni vyema jamii ikaendelea kujenga amani na kudumisha mashirikiano yaliyopo nchini.
Waziri Haroun ameyasema hayo huko Zanzibar Beach Resort wakati wa ufungaji wa Kongamano la Pili la Kitamatafa la Amani, amesema kudumisha amani ni jambo la msingi katika kutekeleza majukumu na kuleta maendeleo.
Ameeleza kuwa maridhianio yaliopo yameleta mafanikio makubwa nchini kwani yameweza kuleta umoja, mshikamano na kuunganisha udugu wa kihistoria katika jamii ya wazanzibari ambayo duniani kote imelifurahia jambo hilo.
Waziri Haroun amesisistiza kuidumisha amani ndani na nje ya nchi ili Zanzibar ibaki kuwa na historia yenye amani na utulivu na kigezo kwa wengine.
Pia Waziri Haroun amewashukuru marafiki wa Zanzibar kuweza kuilinda na kuidumisha amani nchini na kuwataka kuendelea kuiunga mkono katika kuleta maendeleo.
Mapema akiwasilisha Mada ya Vijana baada ya Uchaguzi Mwezeshaji Sheikh Ibrahim Lethome Wakili kutoka Mahkama Kuu ya Kenya amesema vijana ni lazima walelewe katika maadili mazuri ya dini na kupewa fursa ili kuepukana na ushawishi wa kiasiasa na kuwa mabalozi wazuri wa kudumisha amani.
“Utaratibu wa kuwalea vijana lazima vijana walelewe katika misngi ya dini, wawe na huruma, jasiri na kuutumia vizuri ujana wao wawe na subira, vijana pia wapewe fursa za kujiendeleza kimaisha” alifahamisha Mwezeshaji huyo.
Nae Mwezeshaji Ramadhan Haula akitoa mada ya Mchango wa Vyombo vya Habari katika kulinda amani na utulivu amesema vyombo vya habari vina uwezo mkubwa wa kudumisha amani kwani ni kifaa kinachofikisha ujumbe kwa jamii na kutoa matukio mbalimbali yanayotokea duniani.
Amefahamisha kuwa chombo cha habari ni chombo chenye kutoa mawasiliano na jamii hivyo kinaushawishi mkubwa wa kudumisha ama kuvuga amani ni lazima vitumike vizuri katika kudumisha amani na utulivu nchini.
Kongamano hilo la Kimataifa la siku mbili ambalo limeshirikisha nchi marafiki wa Zanzibar ikiwemo Mozambique, Malawi, DR Congo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya Tanzania Bara, Norway, Switzierland na Germany
No comments:
Post a Comment