Habari za Punde

Kuapishwa Kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Ukumbi wa Ikulu leo 19-3-2021

JAJI Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma akimuapisha Mhe Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo 19-3-2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hasaan katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam (kulia kwake) Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndgugai wakifuatilia hafla hiyo. 
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisaini Hati ya Kiapo baada ya kumaliza kula kiapo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Prof Ibrahi Hamis Juma akisaini hati ya kiapo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe.Samia Suluhu Hassan baada ya kumaliza kula kiapo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.   
MARAIS Wastaaf wa Tanzania kulia Rais Mstaaf wa Awamu ya Pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Tanzania Awamu ya Nne Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Sita Mhe.Dkt. Amani Karume na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Mzee Philip Magula, wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
RAIS wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam,kupokea salamu ya heshima kutoka kwa Gwaride maalum la JWTZ, baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipokea Salamu ya heshima kutoka Gwaride Maalum la jwtz lililoandaliwa katika viwanja vya Ikulu baada ya kuapishwa lililofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
GWARIDE Maalum la Jishi la Wananchi Tanzania JWTZ wakitowa salamu ya heshima kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, lililofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.   
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum la JWTZ baada ya kupokea Salamu ya heshima katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akielekea katika ukumbi wa Ikulu baada ya kumaliza kukagua Gwaride Maalum na kupokea Salamu ya heshima, akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Bashiru Ally.
RAIS Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo 19-3-2021 na (kulia kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam na (kulia kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi,Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai , Jaji Mkuu wa Tanzania MheProf. Ibrahim Hamis Juma na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Bashiru Ally.
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Wananchi baada ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakati akizungumza na Wananchi baada ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam na (kulia kwa Rais) Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ,Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Prof Ibrahim Hamis Juma
MARAIS Wastaaf na Wageni waalikwa wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza baada ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam na (kulia kwake) Mke wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Siti Mwinyi na (kushoto kwake) Mke wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Mama Shadya Karume.

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Spika Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Prof Ibrahim Hamis Juma, baada ya kumaliza kuzungumza na Viongozi na wageni waalikwa baada ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.