Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais akutana na uongozi wa SIMS Hospital ya India

Mkurugenzi Mkuu wa SIMS Hospital Bw. Galal Ahmed akimuelezea Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar juu ya adhma ya Hospital yao kuendelea kutoa tiba kwa wagonjwa mbali mbali Zanzibar.
Dk. Aswin Sayiram wa SIMS hospital akimuhakikishia Mhe. Hemed juu ya uwezo wa hospital yao katika kuendesha Operesheni mbali mbali pamoja na kutibu magonjwa sugu ya binadamu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed akitoa shukrani kwa niaba ya serikali kutokana na mchango mzuri unaotolewa na Hospial ya SIMS ya India katika kuimarisha Afya za wagonjwa wa Zanzibar wanaopatiwa tiba katika hospital hiyo.

Na Kassim Abdi, OMPR

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na India katika  sekta ya Utabibu kwa kuimarisha Afya za wananchi wake.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo wakati akizungumza na viongozi wa hospital ya SIMS ya India Afisni kwake Vuga jijini Zanzibar.

Alisema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza ushirikiano wake na hospitali hiyo kutokana na matibabu mazuri yanayotolewa na madktari katika nyanja mbali mbali akitolea mfano magongwa ya moyo, saratani,tenzi dume na magonjwa mengineyo.

“Niseme tu nyinyi wenzetu tayari mumepiga hatua kubwa katika sekta ya Afya serikali yetu itaendeleza ushirikiano kwa lengo la kuwajengea uwezo watu wetu”.

Mhe. Hemed aliwaomba madktari hao kuangalia namna bora ya kupunguza gharama za upatikanaji wa matibabu ili serikali iweze kutoa huduma hiyo kwa urahisi kwa wananchi wake ikizingatiwa kwamba uhitaji wa  matibabu kwa  wananchi ni mkubwa.

Alieleza kuwa, pamoja na hospitali hiyo kutoa matibu yake kwa wagonjwa lakini pia, kuna haja ya kuangalia uwezekano wa kushirikiana na wafanyakazi wa hospital kwa kuwapatia ujuzi kwa lengo la  kuwajengea uwezo madktari ili waweze kutoa huduma katika maeneo mengine.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Mhe. Hemed aliwaeleza viongozi hao kuwa serikali haina uwezo wa kuwapeleka wagonjwa wengi kwa pamoja nchini India kwa ajili ya kupatiwa tiba hivyo, kuna haja ya kuangalia njia bora zitakazosaidia kuwapatia matibabu wagonjwa hapa hapa Zanzibar na serikali itatoa ushrikiano unaohitajika.  

“Serikali yetu haina uwezo wa kuwapeleka wagonjwa wake wengi India kutokana na Gharama, Itakuwa vyema mukifikiria namna bora ya kutoa huduma zenu ili kupunguza gharama hizo” alisema Mhe. Hemed.

Nae, Mkurugenzi Mkuu kutoka hospital ya SIMS Bw. Galal Ahmed Dawood alimshkuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa ushirikiano wanaopatiwa kutoka serikalini  tangu hospital yao ilipoanza kufanya kazi  zake.

Alisema Ushirikiano huo waliopatiwa umepelekea hospital yao kutekeleza vyema majumu yao bila ya  vizuwiwzi vya aina  yoyote.

Aidha, Bw. Galal alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa, uongozi wa hospital ya SIMS katika kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Zanzibar inaangalia uwezekano wa kuleta madktari wake kutoka Nchini India na kufanya matibabu Zanzibar kwa lengo la kuipunguzia gharama serikali.

Akizungumzia sula la kuwajengea uwezo watendajii  Bw. Galal alisema hospital yao imelenga kutoa mafunzo kwa wanafunzi na madktari kwa kuifanya Zanzibar ipige hatua kwa utoaji wa huduma za kitabibu katika ukanda wa Afrika mashariki.

Kwa upande wake Dk. Aswin Sayiram alieleza kwamba SIMS hospitali ina wafanyakazi wenye uweledi katika kutibu magonjwa mbali mbali ikiwemo saratani,matatizo ya figo, kisukari pamoja na uwezo wa kufanya operesheni tofauti.  

 


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.