Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi afanya uteuzi wa Mawaziri kukamilisha safu ya Uongozi kwenye Baraza la Mawaziri

 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  amefanya uteuzi wa Mawaziri katika Wizara zilizomo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said ilieleza kwamba kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini  ya Vifungu vya 42,43(1)(2) na 44 vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 amefanya uteuzi wa Mawaziri.

Walioteuliwa ni Dk. Saada Mkuya Salum ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

Wengine walioteuliwa ni Omar Said Shaaban kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda na Nassor Ahmed Mazrui ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya Habari, Uteuzi huo umeanza leo tarehe 03 Machi, 2021.

Wateuliwa hao wataapishwa kesho siku ya Alhamis tarehe 04 Machi, 2021 saa 4:00 za asubuhi katika Ukumbi wa Ikulu, Zanzibar.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Mwinyi pia, atamuapisha Salum Yussuf Ali Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ambae aliteuliwa tarehe 10 Februari,2021.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.