Habari za Punde

Bei Mpya ya Mafuta Kutoka ZURA Zanzibar.

 Na Mwashungi Tahir   Maelezo       8-4-2021.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA) imefanya mabadiliko ya bei za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Ijumaa ya Tarehe 09-04-2021.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano (ZURA) Mbaraka Hassan Haji huko kwenye ukumbi wa ZURA  ulioko Maisara  wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa umma juu ya mabadiliko ya bei za mafuta zitakazoanza kutumika hapo kesho.

Amesema ZURA inapanga bei kwa kuzingatia mambo yafuatayo ambapo ikiwemo wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations)  katika mwezi Machi 2021 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanyia mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi April 2021.

Pia inazingatia gharama za uingizaji Mafuta katika Bandari ya Dar-es-salaam , thamani ya Shilingi ya Tanzania kwa Dola za Kimarekani , gharama za usafiri, Bima na ‘Premium ‘hadi Zanzibar, Kodi za Serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji waReja Reja.

Hivyo amesema Aina ya mafuta ya Petroli bei ya mwezi wa Machi, 2021 TZS/LITA 2,026, Bei ya Mwezi wa April, 2021 TZS/LITA 2,165 tofauti (TZS)139 ambapo sawa na asilimia 8.86%.

Diseli  bei ya mwezi Machi , 2021 (TZS/LITA 2,041, bei ya Mwezi April, 2021(TZS/LITA 2,124 tofauti 83 sawa na asilimia 4.07%.

Kwa upande wa Mafuta ya Taa Bei ya mwezi Machi ,2021 (TZS/LITA 1,471 bei ya Mwezi April ,2021(TZS/LITA 1,471 tofauri 0 sawa na asilimia 0.0%.

Mbaraka amesema Bei za bidhaa za mafuta ya Petroli na Dizeli katika mwezi wa April , 2021 zimeongezeka , wakati bei za bidhaa ya mafuta ya taa haikubadilika ikilinganishwa na bei za bidhaa hizo katika mwezi wa Machi,  2021 kutokana na kubadilika kwa wastani wa bei za uuaji wa bidhaa hizo katika Soko la Dunia pamoja na soko la ndani kwa kupitia bandari ya Dar es salaam.

Hivyo ZURA inapenda kuwajuilisha wananchi kuwa bei zilizotangazwa ndio bei halali zitakazoanza kutumika siku ya Ijumaa Tarehe 09/04/2021.

Pia amewaomba wananchi wanapokwenda kununua bidhaa hizo wadai risiti na wanapokutwa na changamoto ikiwemo huduma za mafuta, maji  na gesi wawasiliane na ZURA ili waweze kutatuliwa changamoto zao.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.