Habari za Punde

Bi Maryam mwananmke wa mfano Zanzibar.

Mjasiriamali wa Ufinyazi Maryam Issa Khamis akishika Chungu Jiko kilichotengenezwa na Wanawake kutoka Kikundi cha Kamba Ndefu huko Fuoni Mambosasa Wilaya ya Magharib ‘B’.
Muonekano wa Mjasiriamali Maryam Issa Khamiss akionekanwa kavaa Baadhi ya Bidhaa zilizotengenezwa na Wanawake kwa kutumia Mikono ikiwemo Mkoba wa Ukili na Kofia akiwa ameshikilia Chombo aina ya Chungu Jiko huko Mapinduzi Squre katika Banda lake la Maonyesho ya Wajasiriamali.
Baadhi ya Bidhaa za ufinyanzi zilizotengenezwa kwa  kutumia Udongo kwa ajili ya matumizi ya Majumbani na Wajasiriamali Wanawake kutoka Kikundi cha Kamba Ndefu kilichopo Fuoni Mambosasa Mkoa wa Mjini Magharibi  .

Na Maryam Kidiko /  Maelezo  Zanzibar. 

“Moja ya biashara iliyonikomboa katika maisha yangu ni biashara ya kuuza Ndimu, ambayo nilianza nayo kama masihara , lakini imeweza kunipatia fedha nyingi hadi kufikia kumiliki nyumba moja na kiwanja”.

 

Hiyo ni kauli ya Mjasiriamali Maryam Issa Khamis mkaazi wa Fuoni Mambosasa, aliyezaliwa miaka ya 77 na ana umri wa miaka 44 kwa sasa, ambae ni Mjasiriamali wa Ufinyazi wa Vitu mbali mbali vya asili (African Tools food and buys Prodaction).

 

Maryam ameanza harakati zake za ujasiariamali akiwa na umri wa miaka 13, miaka ya 1990, wakati huo alieleza kwamba akisoma Skuli ya Lumumba, ambapo wakati huo alikuwa akiuza biashara ya Uji, Supu huko Mbweni Chuo cha Ufundi Karume nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

 

Mwaka 2004 Bimaryam aliolewa ndoa yake ya kwanza lakini hakutaka kuwa mama wa Nyumabi tu bali aliamua kujishuhulisha na Ushonaji wa Madira,Foronya,Mito Pamoja na Magunia ya kufutia Miguu.

 

Mnamo miaka ya 2011 Bi Maryam aliamua kufanya Biashara ndogo ndogo kama vile Ndizi,Nyanya,Mabilinganyi kadhalika, alikua akitumia soko la Mwanakwerekwe .

Baada ya hapo aliamua kubadilisha biashara mnamo miaka ya 2014 / 2015  na kuanza biashara ya kuuza Dagaa akiwa anasafirisha Tanzania Bara.

 

Katika harakati zake hizo za kuuza Dagaa alikutana na mwanamke ambae anauza Vyungu na kununua chungu kimoja ambacho alikujakiuza Zanzibar, Chungu hicho kiliweza kupata Wateja na kuamua kwenda kuchukua vyengine 50.

 

Kutokana na kupata wateja wanaohitaji vyungu hivyo , aliamua kufunga safari hadi Tanzania Bara kwa kujifunza utengenezaji wa Vyungu hivyo ili  kulimiliki soko vizuri .

 

Baada ya kujifunza mnamo mwaka 2016 alikuwa na uwezo wa kutengeneza mwenyewe na kuamua kufungua kikundi kinachoitwa KAMBA NDEFU kikiwa na Wanachama watano.

 

Baada ya hapo aliamua kujiongeza zaidi kwa kufanya vyungu vya aina mbali mbali vya kutumia kikiwamoo chungu maalum ‘Chungu jiko’  na vitu vyengine ambapo kikundi hicho kimeanzisha duka na kuuza vitu vyao wanavyotengeneza.

 

Alisema kuwa Shirika la Utangazaji Zanzzibar (ZBC) limemuwezesha kukitambulisha Chungu jiko chake kwa kutengeneza akionyeshwa live na watu wengi kuona .

Vile vile alipata kutengeneza vyungu vingi na kuuza katika tamasha la nanenane na kupata faida kubwa kwa kujitokeza kwa watu wengi kununua vyungu na bidhaa za asili anazouza ikiwemo Mbuzi ya kukunia nazi, Mashanuo, Mikoba ya Ukili n.k.

 

Hata hivyo alishiriki katika shindano la Tamasha la sherehe za Mapinduzi la Mjasiriamali mbunifu na kutokea mshindi wa pili Nakupata zawadi ya pesa shilingi laki tano taslim za Tanzania ambapo chungu jiko ndio kilichomfanya ashinde baada ya kukitambulisha katika Tamasha hilo.

 

Aidha alisema katika Kikundi hicho wanashirikiana vizuri na Wanawake wenziwe na kuuza biashara zao kwa Jumla na Rejareja sehemu mbali mbali ikiwemo  Wamachinga,wanouza kwa baskeli,madukani na maeneo mbali mbali husan kukitokea maonyesho ya biashara na ujasiriamali.

 

“Sikatika kikundi tu mashirikiano mazuri napata katika familia yangu wananiunga mkono vizuri ninapotokezewa na matatizo nikiwa katika safari nikihitaji msaada hupata mara moja’’.alisema Maryam Issa.

 

Katika kipindi chake chote bi Maryam alipata faida katika biashara zake na kufikia  kupata Viwanja Viwili kujenga nyumba moja maeneo ya Fuoni mambosasa ambako ndipo anapokaa.

 

Pia faida nyengine aliyoipata ni kumsomesha mwanawe Skuli kuanzia Msingi hadi Sekondari mpaka sasa kupitia mradi wake huo anauwezo wa kujikimu mahitaji yake madogomadogo na kuwasaidia Familia yake.

 

Panapofaida na hasara hazikosi hivyo bi Maryam alisema kuna changamoto kutopata Mashirikiano Baadhi ya sehemu wanazoenda kwa lengo la kuitangaza biashara yao zaid kama Semina na Mahoteli ikiwa ni sehemu kubwa ya Watalii.

 

Vile vile anapotaka kushiriki katika maonesho ya Nje ya  Nchi hua hawezi kushiriki kutokana na uzito wa biashara yake ya vyungu na kuvunjika kutokana na kukosa vifaa vya kuhifadhia.

 

“Serikali hairuhusu bidhaa zetu kuzihifadhi kwa majani au nyasi kutokana na kuwa ni hifadhi ya taifa, hivyo ushiriki wa maonesho ya nchi tunatamani tuu”alisema.

 

Hata hivyo alisema lengo kubwa la kuwa mjasiriamali wa ufinyazi nikuenzi utamaduni wa kutumia vitu vya asili ambavyo vinasaidia kiafya kwa watumiaji kwani  ni vitu vya Udongo vinavyotumika kwa matumizi ya nyumbani ya kila siku.

 

Pia anahitaji kushiriki mashindano makubwa zaidi mbali na yanayofanyika Zanzibar na Tanzania bara kwa lengo la kuzidi kutimiza malengo yake.

 

“Wapo watu wanasema Wanawake hatuwezi lakini tunaweza, Wanawake wengi hivi sasa wanaelimu ya Ujasiriamali wa kazi za Mikono na kupelekea Wanawake ni nguzo muhimu sana katika kila Nyanja na kupata fursa ya kuwasomesha Wanawake wenzao”.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.