Habari za Punde

Chama Cha Viziwi Wilayani Korogwe Watowa Warsha ya Kujadili Upatikanaji wa Takwimu ili Kuboresha Huduma za Afya.

Washiri wa Warsha ya kujadili upatikanaji wa Takwimu ili kuboresha huduma ya Afya  ambao ni madaktari wa vituo vya afya wilayani korogwe wakifuatilia warsha hiyo.
Na Hamida Kamchalla, KOROGWE.

CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) wilayani Korogwe mkoani Tanga kimeendelea kutoa mafunzo ya lugha za alama elimu hii iliopatikana itumike kwa watoa huduma pindi wakiwepo vituoni kuwadudumia watu wenye uziwi.

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la The Foundation for Civil Society (Fcs), yanalenga kuwahakikisha watu wenye ulemavu wanapata takwimu au taarifa ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati ya huduma za afya ipasavyo pasi na kutwengwa au kunyanyapaliwa.

Akiongea wakati wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa CHAVITA wilaya ya Korogwe Happyness Kuboja alisema kuna wakati wanapata matatizo makubwa wanapofika katika vituo vya kutolea huduma za afya kiasi cha kushindwa kupata matibabu.

“Tumekuwa tukipata kero nyingi sana tunapokwenda kupata huduma za afya kutokana na wahudumu kutokuelewa lugha za alama jambo linalotupelekea wakati mwingine kukosa huduma na kuishia kurudi nyumbani huku tunaumwa” alisema Kuboja.

“Lengo kubwa lamafunzo haya ni kuwaelimisha wahudumu wa afya jinsi ya kuwasiliana, kuwapokea na kuwahudumia wenye ulemavu wa kusikia na wengineo  wakati wanapofika kupata huduma” aliongeza.

Kuboja aliiomba serikali kutenga bajeti ambayo ni endelevu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa wahudumu katika taasisi zote ili kuweza kuwajenga kimawasiliano na kuondoa dhana potofu inayopelekea wenye ulemavu kuonekana ni watu wasiofaa kwenye jamii.

Naye Katibu wa chama hicho ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa mafunzo hayo Ally Nassoro alisema mafunzo hayo ya siku mbili ni kwa wahudumu wa afya pekee lakini pia wataendelea kuyatoa kwa wahudumu wengine ili kuweza kujenga wigo mpana wa mawasiliano kati ya wenye ulemavu na wasio nao.

Nassoro alifafanua kwamba kwa kufanya mafunzo hayo wataweza kuondoa hali ya unyanyapaa kwa wenye ulemavu wanapokwenda kutibiwa na pia kuwapa nafasi ya kuendelea na majukumu yao mengine ndugu wanaohitajika kuwasindikiza kupata huduma.

“Tunajaribu kuwaelimisha wahudumu kuzoea kuongea na walemavu kama viziwi na mabubu ilikuacha tabia ya kuwadharau pindi wanapokwenda kupata huduma na ikiwezekana kuwapa kipaumbele kupishwa kupata huduma kabla ya wasio na ulemavu” alisema.

Pia aliwataka wale wote wanaojifunza lugha za alama kuzisambaza kwa watu wengine ili iweze kuenea kwa urahisi kwakuwa itaifanya jamii kuona hakuna utofauti kati ya wenye ulemavu na wazima.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.