Na Miza Kona Maelezo Zanzibar. 20/05/2020
Maafisa Habari na Uhusiano wametakiwa kuelimisha jamii kuhusiana na huduma zinatolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) ili kuzijua na kuzitumia ipasavyo.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Hassan Juma Amour katika mkutano wa Mwaka wa Wadau wa ZURA uliofanyika huko Ofisini kwao Maisara wa kujadili majukumu ya Mamlaka, mafanikio, changamoto pamoja na mipango yake katika miaka ijayo
Amesema Maafisa Habari na Afisa Uhusiano ndio wadau wakuu wa kutoa na kufikisha taarifa kwa jamii kwa urahisi pamoja na kuweza kuzitumia huduma na kuibua changamoto zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ili kuepukana na athari zinawowezakujitokeza.
Ameeleza kuwa ZURA inajukumu la kusimamia huduma za maji na nishati zinatolewa kwa uwazi na ufanisi ili kukuza uwekezaji na kuchangia maendeleo ya kiuchumi nchini.
Amefahamisha kuwa ZURA imefanikiwa kuandaa kanuni na miongozo ya Mafuta ,Umeme na Maji ili kumlinda mtumiaji pamoja na kutambulisha utaratibu mpya wa leseni kwa vituo vya Mafuta na Gesi.
Akielezea changamoto inayoikabili taasisi hiyo ni pamoja na uelewa mdogo juu ya majukumu ya Mamlaka kwa taasisi zinazodhibitiwa na ZURA pamoja na kuibuliwa kwa maombi mengi ya kuanzishwa kwa vituo vipya vya maji.
No comments:
Post a Comment