Habari za Punde

Mwenge wa Uhuru Wawasili Kisiwani Pemba Ukitokea Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Baada ya Kumaliza Mbio Zake Mkoa huo leo.

MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi  Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa, akisoma taarifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 kutoka mkoa huo kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, makabidhiano ya Mwenge huo yamefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Chakechake Pemba.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Mattar Zahor Masoud kushoto) akipokea mwenge wa uhuru kitaifa 2021 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana kwa ajili ya kuukimbiza katika Wilaya ya Mkoani na Wilaya ya ChakeChake Mkoa wa Kusini Pemba,ukitokea Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja baada ya kumaliza mbio zake Mkoani huo.

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Mattar Zahor Masoud (kulia) akimkabidhi Mwenge wa uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba Mhe.Issa Juma Ali (kushoto) kwa ajili ya kukimbizwa ndani ya wilaya hiyo, ambapo utazindua miradi mbalimbali, kukagua na kuweka jiwe la msingi miradi tisa yenye thamani ya shilingi 240,926,047/=.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Mattar Zahor Massoud (mwenye miwani) akiwaongoza watendaji mbalimbali wa serikali Kisiwani Pemba, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Salama Mbarouk Khatib, katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kitaifa 2021 kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
MWENGE wa Uhuru ukiwa umewasili katika uwanja vya ndege kisiwani Pemba, ukitokea Mkoa wa Mjini Magharibi na kuukabidhiwa kwa Mkoa wa Kusini Pemba kwa kuanza kukimbizwa kwenye wilaya ya Mkoani

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.