Habari za Punde

Waathirika wa Masterlife watakiwa kuwa na subira huku suala lao likitafutiwa ufumbuzi

Mwenyekiti wa kamati maalum ya  waathirika wa uwekezaji katika Kampuni ya Masterlife Thabit Mohammed Saleh akizungumza na wahanga wa kampuni hiyo juu ya suala zima la mwendelezo wa kudai haki yao kisheria huko katika Ukumbi wa Taqwa Mlandege Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa kamati maalum ya  waathirika wa uwekezaji katika Kampuni ya Masterlife Thabit Mohammed Saleh akizungumza na wahanga wa kampuni hiyo juu ya suala zima la mwendelezo wa kudai haki yao kisheria huko katika Ukumbi wa Taqwa Mlandege Mjini Zanzibar.

 Waathirika mbalimbali wa Uwekezaji katika Kampuni ya Masterlife wakifuatilia kwa makini kikao cha kamati ya waathirika hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Taqwa Mlandege Mjini Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA / MAELEZO ZANZIBAR.


NA SABIHA KHAMIS / MAELEZO ZANZIBAR 27.05.20-21

Mwenyekiti wa kamati maalum ya  wahanga wa uwekezaji katika Kampuni ya Masterlife Thabit Mohammed Saleh  amewataka waathirika wenziwe kuwa na busara pamoja na subra katika kipindi hiki kugumu cha kudai haki zao .

Akizungumza na wawekezaji hao katika Ukumbi wa Taqwa uliopo Mlandege Mjini Zanzibar, amesema Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi bado anaendelea kulifanyia kazi suala la kutafuta haki za kila mwekezaji ndani ya Kampuni hiyo.

Amewaomba wawekezaji hao waendelee kuwa na imani na raisi wa Zanzibar kwani ameahidi kutekeleza jambo hilo kwa asilimia mia Na kusisitiza kuwa adhma yake ni kuona kila mwanachma wa Masterlife anapata haki yake aliyoiwekeza.

Kwa pamoja kamati imeahidi kutoa taarifa kwa wahanga wenzao hatua kwa hatua ili kuondosha utetatinishi juu ya suala hilo.

Nao waathirika wa uwekezaji huo wameahidi kuendelea kuwa pamoja na Rais wa Zanzibar ili kumpa nguvu katika kutekeleza wajibu wake wa kutetea haki za  kila mwananchi.

Kampuni ya Masterlife ina jumla ya wanachama kumi na moja elfu waliowekeza katika kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.