Habari za Punde

Watendaji wa Taasisi Zinazoshughulikia Rasilimali Watu Kutekeleza Majukumu Yao.

Na Khadija  Khamis –Maelezo Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame amewataka watendaji wa taasisi zinazoshughulikia rasilimali watu kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kuepukana na matukio ya hatari.

Ameyasema hayo wakati akikagua Bandari ya Malindi Zanzibar wakati w kuchunguza vyombo vinavyosafirisha abiria pamoja na maeneo wanaokaa abiria hao.

Alisema kuwa ni vyema wafanyakazi kupewa mafunzo ya kukabiliana na maafa kwani imeonyesha hawana uelewa wowote pindipo  maafa yakitokea .

Aidha aliwataka wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini (ZMA) kuweka utaribu mzuri wa usalama wa abiria na mali zao kwani imeonyesha hata sehemu ya dharura haipo pindi tatizo likitokea .

Alifahamisha kuwepo na mpangilio mzuri  wa kushusha abiria na magari kwani inaonyesha usumbufu mkubwa kwa abiria wanaosafiri.

Hata hivyo amewaeleza Wafanyakazi wa Mamlaka ya usafiri baharini kusimamia vyombo ambavyo havifuati utaratibu uliowekwa na kuvichukulia hatua za kisheria pindi wakikiuka maagizo waliyopewa .

“Haiwezekani vyombo kupakia abiria kupita kiasi huku wakifukuzana baharini jambo ambalo linahatarisha maisha ya watu na mali zao ,tukipoteza rasilimali watu tunapoteza nguvu kazi wa Taifa ,”alisema Mkurugenzi wa Maafa .

Alisema liwepo suala zima la mawasiliano na mashirikiano kwa wafanyakazi ili kuwe na mabadiliko kwa lengo la  kuziondosha changamoto zilizopo .

Alisema kuwa Ukaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria NO. 1 ya mwaka  2015  ya Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa kutoka kwa Makamo wa Pili wa Rais.

Ukaguzi huo ulishirikisha Taasisi mbali mbali zilizomo kwenye Mpango Kazi wa Kukabiliana na Maafa ikiwemo Kikosi vya ulinzi na usalama ,Kikosi Maalum ya Kuzuia Magendo (KMKM) Kikosi Cha Zimamoto .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.