Habari za Punde

Mhe Hemed azifariji familia za Marehemu kufuatilia ajali ya Basi iliyotokea leo alfajiri Mkoani Shinyanga

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itagharamia mazishi ya marehemu waliofariki kufuatia ajali ya Basi lililokua likitikea Nchini Uganda kueleke Dar es Salam.

Mhe. Hemed ameleza hayo wakati akizifariji Familia za Marehemu wao walipofika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ulipo Kisauni nje kidogo ya jijini la Zanzibar.

Amesema serikali inatoa pole zake za dhati kwa Familia za Marehemu pamoja familia zilizopatwa na majeruhi ambao bado wanaendelea kupata matibabu katika spital jijini Shinyaga na wengine kupatiwa rufaa kwenda Spital ya Bugando Jijini Mwanza.

Makamu wa Pili wa Rais amesema serikali imeguswa na msiba uliowapata wanafamilia hao pamoja na majeruhi kitendo kilichopelekea serikali kuchukua hatua za haraka kwa kutoa usafiri  kuwaagiza watendaji kwenda kufuatilia majeruhi na kuzisafirisha maiti hizo kwa ajili kuzikanidhi kwa Familia zao.

Amesema serikali imejipanga kushiriki katika shughuli za mazishi kwa kujipanga katika kila eneo la msiba ili kushirikiana na familia katika kuisitiri miili ya marehemu.

Mhe. Hemed wakati akizifariji familia hizo ametoa salamu za pole kutoka kwa  Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kusema kuwa Mhe. Rais yupo pamoja na familia hizo katika kipindi hiki kigumu na amezitaka ziwe na subra.

"Mhe. Rais anakupeni pole sana kwa msiba huu wa kuondokewa na wapendwa na serikali itagharamia shughuli za mazishi " Alisema Makamu wa Pili.

Makamu wa Pili wa Rais amesema Marehemu hao ambao walikuwa ni wanafunzi wa Kada ya Afya katika chuo cha BUGEMA UNIVERSITY Kampala Nchini Uganda wamelitumikia Taifa kwani wengi wao walikuwa ni watumishi wa Serikali.

"Marehemu hawa walikuwa ni watiifu kwani wametoa mchango mkubwa kwa Taifa kupitia kada zao walizokuwa wakizifanyia kazi" Alieleza Mhe. Hemed 

Marehemu hao wamewasili katika kiwanja cha Ndege cha Abeid Karume majira ya Usiku na kukabidhiwa kwa Familia zao kwa ajili ya taratibu za Mazishi.

Marehemu hao ni 

Rehema Haji Juma - Kizimkazi

Wahda Yussuf - Kwahani na

Nassor Juma Khamis - Bububu.

Viongozi mbali mbali wakiwemo mawaziri na watendaji wengine wa serikali wameshiriki katika shughuli ya kuipokea miili ya Marehemu hao.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Juni 02, 2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.