Habari za Punde

Ufunguzi wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Udhalilishaji Zanzibar.

MKURUGENZI wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania-Zanzibar Dr.Mzuri Issa, akitoa maelezo mafupi katika mkutano wa kushirikishana kuhusu hatua za utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa kupambana na udhalilishaji Zanzibar 2017/2022 uliofanyika katika ofisi za Tamwa Mkanjuni Pemba
MRATIBU wa TAMWA Zanzibar upande wa Pemba Fat-hiya Mussa Said, akiwasilisha ripoti ya utafiti mdogo wa muonekano na Utendaji wa Mahakama maalumu ya kushughulikia udhalilishaji, kwa wadau kutoka taasisi mbali mbali zinazoshuhulika na masuala ya udhalilishaji Pemba, mkutano Uliofanyika katika ofisi za chama hicho Mkanjuni Pemba.
MKUU wa Idara ya jinsia na watoto Pemba Mwanaisha Ali Massoud, akifungua mkutano wa siku moja kwa niaba ya Afisa Mdhamini Wizara ya afya ustawi wa jamii wazee jinsia na watoto, mkutano uliofanyika katika ofisi za TAMWA Pemba.

WADAU kutoka taasisi mbali mbali zinazoshuhulika na masuala ya udhalilishaji wa wanawake na watoto Pemba, wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa ripoti mbali mbali za uzalilishaji, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania/Zanzibar kwa upande wa Pemba.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.