Habari za Punde

Wananchi Watakiwa Kuunga Mkono Juhudi za Viongozi Wakuu wa Nchi Katika Kuijenga Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe, Ithman Masoud Othman akiitikia dua baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Raudha Daraja Bovu Wilaya ya Magharibi "A"Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Masjid Raudha baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid hiyo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, amewasihi wananchi kuendeleza umoja, amani na mshikamano kwa lengo la kuunga mkono juhudi za viongozi wakuu wa nchi katika kuijenga Zanzibar yenye uchumi imara.

Ameyasema hayo mara baada ya kumaliza ibada ya Sala ya Ijumaa katika Masjid Raudha uliopo eneo la Daraja Bovu kisiwani Unguja, ambapo aliwaeleza waumini wenzake kwamba katika kufikia malengo ya serikali, ni vyema wakajikita katika kuyasimamia masuala ya haki, uwajibikaji na uadilifu kwani ndiyo yanayoliinuwa taifa.

Aidha, Alhaj Othman, amewakumbusha waumini hao historia ya msikiti huo katika uhamasishaji wa amani na mshikamano nchini na kuwataka kuiendeleza kwa kujenga taifa lililokuwa imara.

Naye Khatib wa msikiti huo, Sheikh Ali Faki, aliwahimiza waumini hao kuendelea kusimamia mambo ya kheri ili iwe ni sababu ya kupata malipo mazuri kwa Mwenyezi Mungu.

Wananchi Watakiwa 
*Kitengo cha Habari*
*Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar*

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.