Habari za Punde

Wilaya ya Magharibi "A" Imeripotiwa Kuwa na Matukio Mengi Ukilinganisha na Wilaya Nyengine.

Na Mwashungi Tahir     Maelezo    16-6-2021.

Imeelezwa kwamba jumla ya matukio 66 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Mei, 2021 wengi wao walikuwa ni watoto ambao ni asilimia 87.9na wanawake asilimia 12.1.


Akiwasilisha kwa waandishi wa habari  takwimu za ukatili  na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto Mei, 2021 Mkuu wa Serikali katika kitengo cha makosa ya jinai, Madai na jinsia huko katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Bi. Ramla Hassan Pandu amesema idadi ya matukio kwa mwezi imepungua kwa asilimia 38.9 kutoka matukio 108 kwa mwezi wa April,2021 hadi 66 mwezi Mei,2021.


Amesema Wilaya ya Magharibi “A”imeripotiwa kuwa na matukio mengi ukilinganisha  na wilaya nyengine matukio 15 ikifuatiwa na Wilaya ya Wete matukio 10. Wilaya ya Kaskazini 

“A”na Kaskazini “B”imeripotiwa kuwa na idadi ndogo zaidi ya matukio kuliko zote matukio mawili kwa kila wilaya.


Hivyo amesema Wilaya ya Magharibi “A”ilikuwa ina idadi kubwa ya matukio ya kubaka ikilinganishwa na Wilaya nyengine, ambapo jumla ya matukio ya kubaka 11 asilimia 25.6 , kwa upande wa wanawake matukio 4ya kubaka asilimia 9.3 na matukio 39 ya wasichana sawa na asilimia 90.7 yameripotiwa kwa mwezi Mei, 2021.


Ameeleza kwamba matukio 62 yapo chini ya upelelezi wa Polisi na matukio 4yapo katika hatua nyengine , matukio mawili 2 yapo mahakamani, matukio mawili2 yapo Ofisi ya Mashtaka.


RAMLA amesema matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ambayo yameainishwa katika matukio makuu 6 nayo kubaka,kulawiti, kuingilia kinyume na maumbile, kutorosha , shambulio la aibu/kukashif na shambulio.


Nae Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Kaimu Mkuu Idara ya Ustawi wa jamii na wazee Nasima Haji Chum amewataka wazazi na walezi kuzidisha bidii zaidi katika kuwalinda watoto ili waweze kuepukana na vitendo viovu ikiwemo kulawitiwa na kubakwa.


Kwa upande wake wakili wa Serikali wa DPP Khamis Othman Abdulah ameiomba jamii kushirikiana katika malezi  ya watoto kwani mtoto wa mwenzio ndio wako ambapo hata Serikali ya awamu ya nane inahimiza kurudisha malezi ya zamani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.