Habari za Punde

Benki ya NMB Yakabidhi Vifaa vya Ujenzi Kituo cha Afya Jangombe Zanzibar.

MENEJA wa Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar Ndg.Donatus Richard akizungumza na kutowa maelezo ya utekelezaji wa malengo ya Benki yao ya NMB kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja na kukabidhi Vifaa vya Ujenzi Mabati na Mbao kwa ajili ya kuezekea Kituo cha Afya Jangombe, vilivyotolewana Benki ya NMB
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar Ndg.Donatus Richard, akizungumza na kutowa maelezo ya utekelezaji wa Benki ya NMB kusaidia Miradi ya Kijamii,kabla ya kukabidhi msaada wa Mabati na Mbao kwa ajili ya kuezeka Kituo cha Afya Jangombe yaliotolewa na Benki ya NMB.
MAOFISA wa Benki ya NMB MenejaMahusiano Biashara ya Serikali na NMB.Bi.Irehe Masaki na (kulia) Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar.Naima Shaame,  wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakihutubia Wananchi wa Jimbo la Jangombe akiwa katika ziara yake kutembelea utekelezaji wa Miradi ya Maenfdeleo katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Jangombe wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutembelea utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, katika Mkoa huo
MENEJA wa Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar Ndg.Donatus Richard akifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Jangombe wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Mjini akiwa na Meneja Mahusiano Biashara ya Serikali na NMB Bi. Irene Masaki (kulia kwake) na (kushoto kwake) Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar.Bi.Naima Shaame, katika hafla hiyo Benki ya NMB imekabidhi Vifaa vya Ujenzi kwa Kituo cha Afya cha Jangombe Mabati na Mbao
WANANCHI na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya Jangombe wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wananchi na Wafanyakazi wa Kituo hicho wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja na kukabidhi Gari ya Wagonjwa kwa Hospitali ya KMKM ya Masingi na kukabidhiwa Vifaa vya Ujenzi wa Kituo hicho Mbao na Mabati vilivyotolewa na Benki ya NMB.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.