Habari za Punde

Matukio ya Picha Kutoka Kisiwani Pemba

MBUNGE wa Jimbo la Kojani ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande, akimkabidhi sadaka ya nyama ya Ngo’mbe mmoja ya mwananchi wa jimbo la Kojani wakati wa skukuu ya Eid-El=Hajj, hafla iliyofanyika Madenjani Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba
WANANCHI wa Kijiji cha Mdenjani Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete, wakisubiri kukabidhiwa sadaka ya nyama ya Ngo’mbe iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kojani kwa ajili ya skukuu ya Eid-El-Hajji.
MBUNGE wa Jimbo la Kojani ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande (mwenye kanzu) akiwa ameshika kamba kuashiria kumkabidhi Ngo’mbe, Rashid Juma kwa ajili ya kuchinja na kwenda kuwagaiwa wananchi katika moja ya kijiji kilichomo ndani ya jimbo la kojani.

MBUNGE wa Jimbo la Kojani ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande (kushoto wa kwanza)akimkabidhi Ngo’mbe Amour Suleimana, kwajili ya kuchinja na kwenda kuwagaiwa wananchi katika moja ya kijiji kilichomo ndani ya jimbo la kojani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.