Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akikabidhi madawati 85 na viti kwa Walimu na Wanafunzi wenye mahitaji maalum yaliotolewa na Shirika la Bima la Taifa (NIC) Tanzania hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akimkabidhi Mwalimu wa Wanafunzi wenye mahitaji maalum Mfano wa Hundi ya Shillingi 1190,000,000/= zilizokusanywa na kupitia mchango maalum uliofanywa na Makampuni ya Bima Tanzania kupitia NIC, makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akikabidhi Fimbo maalum kwa Mwalimu kwa niaba ya Wizara ya Elimu kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji Maalum msaada ambao umetolewa na Makampuni ya Bima kufuatia machango maalum ulioendeshwa na Taasisi hizo.
Kamishna wa Bima Tanzania Bi Khadija Issa Said akielezea Changamoto zinazoyakabili Makampuni ya Bima Nchini katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Bima Zanzibar iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abduwakil Kikwajuni.
No comments:
Post a Comment