Habari za Punde

Wananchi watahadharishwa na kuibuka kwa vitendo vya ukusanyaji fedha kutoka kwa wananchi kwa kigezo cha uwekezaji

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema kuibuka kwa vitendo vya ukusanyaji wa fedha kutoka kwa wananchi kwa kutumia jina la uwekezaji unaoendelea katika maeneo mbali mbali nchini haupo chini ya usimamizi wa Serikali.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango ukusanyaji huo hufanyika ama kwa njia ya fedha taslim au kupitia mitandao.

 

Taarifa hiyo  inawajuulisha wananchi wa Zanzibar kuwa, shughuli hizo ambazo  hufanywa na vikundi vya watu pamoja na baadhi ya Kampuni ikiwemo Kampuniya PAMA FUNDS, Qnet, GAMEAS, WOZUR na nyenginezo sio salama.

 

Hivyo, Serikali inatoa tahadhari kwa wananchi kwamba, ni vyema kujiepusha na ushiriki wa biashara hizo ili kuepusha upotevu wa mali zao.

 


IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.