BAADHI ya wanawake nane (8) kutoka shehia ya
Kiungoni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakisubiri kupatiwa hati
miliki za ardhi zao, mradi wa haki ya umiliki wa ardhi Pemba unaoendeshwa na
Jumuiya ya KUKHAWA kwa ufadhili wa the Foundation for Civil Society, hafla
iliyofanyika katika jengo la MKURABITA kiungoni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKURUGENZI wa Jumuiya ya KUKHAWA Pemba Hafidhi Abdi
Said, akizungumza wakati wa kikao cha kuwakabidhi hati miliki za ardhi wanawake
nane (8) kutoka shehia ya Kiungoni Wilaya ya Wete, hafla iliyofanyika katika
jengo la MKURABITA Kiungoni.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
AFISA Msajili wa ardhi Pemba Yussuf Hamad Kombo,
akiwaonyesha wananchi nane (8) wanawake wa kiungoni, jinsi hati miliki za ardhi
livyokua na ubora zaidi kufuatia kuwa na picha ya mmiliki wa ardhi husika,
hafla iliyofanyika katika jengo la MKURABITA Kiungoni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
AFISA Msajili wa ardhi Pemba Yussuf Hamad Kombo,
akimjazisha saini mmoja ya wamiliki wa ardhi shehia ya Kiungoni Wilaya ya Wete,
ambapo wanawake hao wamepatiwa ardhi zao kupitia Jumuiya ya KUKHAWA Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKURUGENZI wa Jumuiya ya KUKHAWA Pemba Hafidhi Abdi
Saidi, akimkabidhi Aziza Abdalla Ismaili mmoja ya wanawake nane wa shehia ya
kiungoni ambao wamekabidhiwa hati miliki zao, kwa ufadhili wa Jumuiya ya
KUKHAWA Pemba, hafla iliyofanyika katika jengo la MKURABITA Kiungoni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment