Habari za Punde

CCM Mkoa wa Mjini waiomba Serikali kupatia ufumbuzi upandaji wa bidhaa kwani mzigo kwa wananchi wa kipato cha chini

Mjumbe wa Kamati Kuu Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini wa Mjini wakati alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa CCM Amani Mkoa kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa Chama wa Mkoa huo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuimarisha Chama.
Viongozi na Wanachama wa Mkoa wa Mjini wakifuatilia hotuba ya Mjumbe wa Kamati Kuu Mhe. Hemed alioitoa katika Ukumbi wa Amani CCM Mkoa.
Mhe. Hemed akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM Mkoa wa Mjini (Hawapo Pichani) katika Mkutano Mkuu maalum uliofanyika katika Ukumbi wa Amani CCM Mkoa ambapo amewahakikishia wanachama hao kuwa serikali itaendelea kudhibiti mfummko wa Bidhaa Nchini.
 

Na Kassim Abdi, OMPR


Viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini wameiomba Serikali kulipatia ufumbuzi tatizo la kupanda bei za bidhaa ili ili kuwaondoshea mzigo wananchi wa kipato cha Chini.

Rai hiyo imetolewa na Viongozi  na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini kichama katika kikao maalum na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa Mhe, Hemed Suleiman Abdulla kilichofanyika katika ofisi za CCM Amani Mkoa .

Wliesema hali ya sasa kwa bidhaa hasa za chakula hairizishi jambo ambalo limepelekea kuwaumiza wananchi wakitolea mfano kupanda bei kwa bidha ya mkate na mafuta ya kupikia.

Akitoa ufafanuzi juu ya hoja hizo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alisema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wizara husika kwa ajili ya kupanga namna bora ya bei za bidhaa ili zisiwamize wananchi kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema serikali haitomvumilia mfanyabishara yoyote atakaekwenda kinyume na bei elekezi zinazotolewa na Serikali na akiwathibitishia kuwachukukulia hatua wafanyabiashara wanaokwenda kinyume na maelekezo ya serikali.

Akigusia suala la uongozi ndani ya chama Mhe. Hemed aliseam CCM ina taratibu zake za kikatiba za kuwapata viongozi huku akiwataka wanachama kuwa wavumilivu na kusubiri muda wa uchaguzi wa ndani ya chama na kuacha tabia ya kupanga safu.

Kuhusu tatizo la madawa ya kulevya, Mhe. Hemed aliwaomba viongozi hao kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na serikali kuu katika kupambana na kadhia hiyo ili kujenga taifa lenye Afya bora na kupata viongozi bora  wa baadae.

Alifafanua kuwa, Serikali itachukua hatua kali ikiwemo kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria kwa lengo la kuwadhibiti wale wote wanaojihisisha na vitendo haramu vya kuharibu jamii ya wazanzibar.

 

Pamoja na mambo mengine Mhe. Hemed aliikumbusha jamii kurudi katika jukumu lao la msingi la kusimamia malezi bora kwa vijana wao ili kuwaepusha dhidi ya vitendo vya viovu vilivyokithiri katika jamii

Katika Kikao hicho Mhe. Hemed aliwataka viongozi wa majimbo kuepukana na  majungu na fitina na badala yake wafanye kazi kwa kushirikiana pamoja kwa kuwashirikisha vingozi wa serikali na Chama katika ngazi zote wakati wakitekeleza majukumu yao.

Aidha Mhe. Hemed aliwataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele katika kushawishi jamii ili kuendelea kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwa lengo la kuongeza idadi ya wanachama ikiwa ni miongoni mwa jitihada za kukijenga chama.

Nae Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini kichama Ndugu Abdallah Mwinyi alimueleza Mhe. Hemed kuwa Mkoa huo unasimamia vyema utekelezaji wa Ilani hadi sasa, ambapo viongozi wa majimbo wapo karibu na wananchi kutatua kero zinazowakabili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Ndugu Talib Ali alimueleza Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM Taifa kuwa katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kwa mara ya kwanza Mkoa huo kuchukua ushindi wa majimbo yote kwa nafasi zilizogombewa.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.