Habari za Punde

KATIBU MKUU CCM DANIEL CHONGOLO ATOA SIKU 14 KWA VIONGOZI NGAZI YA WILAYA NA MIKOA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI NA TAARIFA IWASILISHWE OFISINI KWAKE

 

Katibu Mkuu wa CCM akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg Masanja Kadogosa mara baada ya kuhitimisha Ziara ya Kukagua Mradi wa SGR alioanzia Mkoani Morogoro hadi jiji la  Dar Es Salaam katika Stesheni ya Mpya ya SGR Tazara.

Katibu Mkuu wa CCM akisikikiza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg Masanja Kadogosa wakiwa safarini kitokea Mkoani Morogoro kuelekea Dar Es Salaam katika treni ya Uhandisi

................................................................................................................
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza viongozi wa chama hasa kupitia Kamati za Siasa katika ngazi za wilaya na mikoa ndani ya siku 14 wakamilishe kukagua miradi yote ya maendeleo ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika maeneo yao na taarifa ya kilichojiri iwasilishwe ofisini kwake.

Sambamba na maagizo ya kuwataka kukagua miradi ya maendeleo, Chongolo pia amewaagiza kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa ilani na amesisitiza kuwa chama kitafuatilia utekelezaji wa maagizo hayo. 

Chongolo ametoa maagizo hayo leo tarehe 10 Agosti, 2021 mkoani Morogoro wakati akikagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa  (SGR), akiwa ameambatana na Wajumbe wa Sekreterieti ya Chama Taifa.

"Niwapongeze watu wa Morogoro kwani mmeweza kuonesha njia nami nimeamka nije hapa na sekretarieti yangu kujionea kama kinachofanyika hapa ni kile kilichoelekezwa katika ilani yetu ya uchaguzi na ndicho kinachoelezwa kila mara,"amesema Chongolo na kuongeza "Haya ni maagizo na maelekezo Kama tulivyopeana mara baada ya mkutano mkuu maalum kuwa wote tushuke chini kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo yetu ."

Amesema wao wanawajibu wa  kuisimamia Serikali na utekelezaji wa Ilani kwani ni sisi ndio tutakaorudi kuwaeleza wananchi nini tumefanya.

Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa amesema anaishikuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa wakati kwa ajili ya kukamilisha mradi huo huku akifafanua mpaka sasa wamelipa  hati 34 kati ya 35 huku hiyo moja ambayo inalipwa muda wowote kuanzia sasa.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031.Wajumbe wa Sekretariet wakiwa katika treni ya Uhandisi kutoka morogoro kihonda hadi dar es Salaam kwanza kulia ni katibu mkuu wa UWT Taifa dkt Philis Nyimbi ,Kenani kihongosi katibu Mkuu wa UVCCM Pamoja na Katibu wa Sekretarieti ya CCM ndg Salum Reja.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakitazama Treni ya Wahandisi kabla ya kuanza Safari kwa kutumia Usafiri huo kutokea Mkoani Morogoro kwenda Mkoa wa Dar Es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo (Kushoto) akifurahia Jambo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe, Martin Shigela  Pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua Stesheni ya SGR Kihonda Mkoani Morogoro.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikaguawakikagua Stesheni ya SGR Kihonda Mkoani Morogoro..

Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakiwa nje ya Handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031.
 (PICHA ZOTE NA CCM MAKAO MAKUU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.