Habari za Punde

Mhe Hemed azindua vitabu vya washairi katika tamasha la kwanza la washairi Tanzania

Baadhi ya washiriki wa Tamasha la kwanza la Washairi Tanzania wakifuatilia Tamasha hilo katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar ambalo lilibeba kauli mbiu isemayo “USHAIRI WA KISWAHILI NI RASILIMALI YETU TUUTUNZE”.
Mshairi Said Sleiman (RUBA) akisoma risala kwa niaba ya Chama cha Kuwaendeleza Washairi Zanzibar (CHAKUWAZA) na  Umoja wa Washairi  Tanzania (UWASHATA) katika hafla ya Tamasha la kwanza la Washairi Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.

Mwenyekiti wa Umoja wa  washairi Tanzania Bara Hassan Lingile akitoa salamu kwa niaba ya washairi wa Tanzania Bara katika hafla ya Tamasha la kwanza la Washairi Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Mshairi Asha Saidi yussuf akiwa na Washairi wenziwe wakifikisha  ujumbe kwa jamii unaohusiana na  umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike, udhalilishaji, na uchumi wa Buluu kwa njia ya tungo za mashairi  katika hafla ya tamasha la kwanza la washairi Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Kuwaendeleza Washairi Zanzibar (CHAKUWAZA) Mussa Makame Dere akimkaribisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo Tabia Maulid Mwita ili amakaribishe mgeni Rasmi kuhutubia katika Tamasha la kwanza la Washairi Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni  na michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza machache na kumkaribisha Mgeni Rasmi Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla kuhutubia katika Tamasha la kwanza la Washairi Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla akihutubia katika Tamasha la kwanza la Washairi Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla akizindua vitabu vya washairi katika Tamasha la kwanza la Washairi Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla (KUSHOTO) akimkabidhi cheti maalum mshairi Maimuna Hashim Maalim kwa niaba ya Chama cha Kuwaendeleza Washairi Zanzibar (CHAKUWAZA)  katika Tamasha la kwanza la Washairi Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.

 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla (KUSHOTO) akimkabidhi cheti maalum mshairi Anthony James Mkema kwa niaba ya  na  Umoja wa Washairi  Tanzania (UWASHATA) katika hafla ya Tamasha la kwanza la Washairi Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA /MAELEZO ZANZIBAR.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.