Habari za Punde

Uzinduzi wa Baraza la Kiswahili la Saba BAKIZA Watakiwa Kutumia Weledi na Taaluma Zao Ili Kulisaidia Baraza.- Waziri Mhe.Tabia.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Bi Mwanahija Ali Juma akitoa maelezo kuhusu Baraza hilo katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Saba la Kiswahili Zanzibar.
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akimkabithi mjumbe mstaafu Mwanaheri Amour Haji  cheti cha kustaafu kwa kufanya kazi katika baraza la Kiswahili wakatiwa uzinduzi wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) .
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akimkabithi mjumbe mstaafu Bwana Haji cheti cha kustaafu kwa kufanya kazi katika Baraza la Kiswahili huko  Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Unguja katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) .
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akimkabithi mjumbe mstaafu Bwana Ameir  cheti cha kustaafu kwa kufanya kazi katika Baraza la Kiswahili huko   Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Unguja katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) .
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) waliyohudhuria katika Uzinduzi wa Baraza hilo uliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Unguja.

Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Picha Na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Na Ali Issa - Maelezo Zanzibar.  14/8/2021

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulidi Mwita amewataka Wajumbe wa Baraza la kiswahili la saba la Zanzibar kutumia weledi na Taaluma zao walizo nazo ili kulisaidia baraza hilo kusimamia vyema lugha ya Kiswahili na Maendeleo yake ndani na nje ya nchi.

Hayo ameyasema katika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Zanzibar wakati akizindua baraza hilo  jipya la Saba ukumbini hapo.

Amesema baraza la Kiswahili BAKIZA linakazi nyingi zilizo bainishwa katika sharia yake ambapo dhamira  kuu ni kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili ndani ya Zanzibar na kufuatilia maendeleo yake Tanzania  na duniani kote kwa lengo la kuandaa program bora zitazo saidia kuendeleza Kiswahili kukua ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Amesema baraza liendelezwe pale walipo acha weziwao ambao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa na wanapaswa kupongezwa.

Aidha amesema waendeleze kazi hiyo kwa maslahi ya Taifa la Zanzibar na ulimwenguni kote ili kuona Kiswahili kinapiga hatua kubwa ya kimaendeleo  siku hadi siku.

Hata hivyo Waziri huyo alieleza kuwa muendelezo utaifanya Zanzibar kuendeleza mambo muhimu ya kuzingatiwa katika kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi na kukuza uchumi wa kisasa na Jumuishi pamoja na ushindani utao jengwa kupitia viwanda,huduma za kiuchumi na miundo mbinu itakayo rahisisha diploma ya kisiasa katika nchi za Afrika mashariki,kusini mwa afrika ,AU SADC,na Umoja wa Mataifa UN kwa kuhakikisha lugha hiyo inafanikiwa kwa vitendo.

Nae mwenyekiti wa baraza hilo jipya Saade Said Mbarouk alimwambia Waziri kuwa wanaelewa Baraza hilo linakazi nyingi lakini watakuwa mstari wa mbele kuona dhamira walio pewa inafanikiwa kwani wanatambuwa Kiswahili ndio kielelezo muhimu katika maisha ya jamii ya kizanzibari na Tanzania kwa ujumla.

Alisema watapaswa kuilinda lugha hiyo kwa hali namali  kukiendeleza,na kushauriana na wezao BAKIZA ili Kiswahili kichukue nafasi yake kwa matumizi mazuri ya lugha hapa na duniani kote.

Nae Mjumbe Mstaafu wa Baraza lililo pita akizungumza kwa niaba yake na weziwe kwa ujumla akitoa neno la shukurani  dkt. Hamad Khamis Juma amesema kuwa siri ya mafanikio ya kufanya vizuri na kufanikiwa kwao ni ushirikiano walio kuwa nao,hivyo baraza jipya waige mfano wao wajenge ushirikiano imara watafanikiwa, na wao wako tayari kutoa mchango wakati wowote watapohitajika.

 Sambamba na hayo Waziri aliwatunuku vyeti wajumbe  wastaafu wabaraza la kiswahili Zanzibar  lililo pita. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.