Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe.Ngasa Ameagizwa Kupeleka Wakaguzi.

Mbunge Ngassa akionyesha kitabu cha Histori kwa wananchi kwa ajili ya masomo kwa wanafunzi  katika shule ya Nanga wilayani Igunga.

Na Lucas Raphael,Tabora.

Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imeagizwa kupeleka  Ukaguzi  maalumu kwa ajili ya matumizi mabaya ya fedha  zenye utata zaidi ya  Milioni 7.

Agizo hilo lilitolewa na Mbunge wa jimbo la Igunga Mkoani Tabora Nicholaus Ngassa wakati akifanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika vijiji vya Kaumbu na Nanga wilayani humo.

Ngassa alisema fedha zlizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho tangu mwaka 2019 kwa ajili ya kuunga mkono nguvu za Wananchi katika kuendeleza , Ujenzi wa Vyoo na Nyumba ya Walimu wa Shule ya Msingi. 


Mbunge huyo alisema  kwamba Kulikuwa na taarifa za matumizi yenye utata Milioni 7,  hivyo tumetoa maelekezo Halmashauri ilete Mkaguzi ufanyike ukaguzi maalum, tulimalize jambo hili, tuendelee na ujenzi.


Katika hatua nyingine Mbunge huyo aliwaeleza wananchi wake kwamba barabara ya Bulyang'ombe - Kaumbu na ile ya Nanga - Kaumbu wameziweka kwenye mpango wa matengenezo. Mwezi Novemba tutazitengea Fedha zijengwa kwa Kiwango cha changarawe.


Ngassa alizungumzia swala la Maji ya Ziwa Victoria yamefika hapo na  kuna magati manane yamejengwa na kuwahudumia wananchi  Kila gati lina uwezo wa kuhudumia Wananchi 1, 000.


Katika ziara hiyo aliwaeleza wananchi wake kwamba wanafanya upanuzi wa kituo cha afya Nanga ili kiweze kukidhi vigezo vya sera ya afya chenye jengo la mama na mtoto , maabara , jengo la upasuaji , jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na nyumba ya mganga.


Alisema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha milion 400 kutoka serikalini kwa ajili ya kukamilisha kituo cha afya na kwa ajili ya hatua zote za upanuzi zinaendelea .


Mbunge huyo alizungumzia  Shule ya sekondari ya Nanga walipata fedha kwa ajili ya ujenzi  wa maabara ya kompyuta katika shule hiyo kongwe itakuwa chachu katika kukuza maarifa ya watoto wao.


Katika shule hiyo inaendelea kufanya vizuri katika ufaulu wa wanafunzi na ni vema ikaendelea kuunga mkono serikali , walimu na wanafunzi katika kuboresha elimu na matokeo.


Akizungumza na wananchi katika kata ya Nanga kijiji cja Bulyang'ombe aliwaambia kwamba wajiandae  kwa fursa za bomba la mafuta la kutoka nchini Uganda (HOIMA) kwenda Tanga ambalo litapitia katika kijiji hicho.


Wananchi wamepata bahati kwa kuwa na kambi (site camp) Kupita kwa bomba hilo kutakuwa na wageni wengi katika kijiji chao ni vema wakajiandaa mapema kutumia fursa hiyo kwa huduma ya chakula na kupata ajira za mikataba.


Aliwataka wananchi hao kuwa waaminifu watakaopewa ajira na wazingatie uzalendo wa nchi yetu kwa kuwa Tanzania kwenye huo mradi tunaumiliki kwa asilimia 15.


Ngassa alisema katika shule za msingi Bulyang'ombe kuna ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo unaendelea baada ya kupatiwa fedha za EP4R na serikali yetu.


Alisema kwa upande wa jengo lililokwama kwa muda  litamalizika na katika vijiji vingine shighuli za maendeleo zinafanyika kupitia serikali hii ya ccm ipo kazini chini ya Rais Samia Suluhu Hassani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.