Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameshiriki Katika Sala ya Kuusalia Mwili wa Marehemu Suleiman Othman Nyanga Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Zanzibar. Kuus

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha Hitma ya Marehemu Suleiman Othman Nyanga, ikisomwa na Ustadh.Abdulrahaman Shariff Al-Habshy, baada ya kumaliza kisomo hicha kabla ya kuusalia mwili wa marehemu katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja. na (kulia kwa Rais) Mtoto wa Marehemu.Mohammed Suleiman Nyanga na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume, Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
Ustadh.Abdulrahaman Shariff Al-Habshy akisoma dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma kumuombea dua marehemu Suleiman Othman Nyanga kabla ya kuusalia mwili wa marehemu katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja na (kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akiitikia dua.
Waumini wa Dini ya Kiislan ndigu na jamaa wa marehemu wakiitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma kumuombea Marehemu Suleiman Othman Nyanga kabla ya kuusalia mwili wa marehemu katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume.(kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Mtoto wa Marehemu Mohammed Suleiman Nyanga na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj Dkt. Amani Karume wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa marehemu iliofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja

Viongozi Wastaaf wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakishiriki katika maziko na Sala ya Marehemu Suleiman Nyanga iliofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja kutoka kushoto Rais Mstaaf  wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaaf wa Alhaj Dkt. Amani Abeid Karume na Makamu wa Pilin wa Rais Mstaaf Alhaj Balozi Seif Ali Iddi. 

WANANCHI na Wauminin wa Kiislam wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu Suleiman Othman Nyanga baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya kuusalia mwili wa marehemi iliofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja.

WANANCHI na Wauminin wa Kiislam wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu Suleiman Othman Nyanga baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya kuusalia mwili wa marehemi iliofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.