Habari za Punde

Serikali tayari imeshaingiza chanjo ya Johnson & Johnson ili wananchi wapate chanjo kujikinga na maradhi ya Covid-19

Waumini  waliojitokeza kuitekeleza Ibada ya sala ya Ijumaa katika Masjid Noor, Muyuni wakimskiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipowasalimia mara baada ya kutekeleza Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwasalimia waumini mara baada ya kukamilika kwa ibada ya sala ya Ijumaa aliojumuika nao katika Masjid Noor uliopo Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.

Na Kassim Abdi, OMPR

Serikali kupitia Wizara ya Afya, ustawi wa Jamii, wazee, Jinsia na watato tayari imengiza chanjo ya Johnson & Johnson ili kuwapa fursa wananchi wake kupata huduma ya chanjo kwa ajili ya kujikinga na maradhi ya Covid-19.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo mara baada ya kutekeleza ibada ya sala ya Ijumaa aliojumuika pamoja na wanachi wa Muyuni katika Majid Noor uliopo Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.

Mhe. Hemed alisema serikali imeamua kuingiza Chanjo hiyo ambayo inatolewa katika Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja ili kuwaondoshea usumbufu waumini wa Dini ya Kiislamu wanaotaka kwenda kutekeleza Ibada ya Umrah Nchini Saudi Arabia.

Aliwataka wananchi kuendelea kujitokeza kupata Chanjo kwa lengo la kujikinga na Maradhi, maradhi ambayo yamekuwa tishio duniani sambamba na kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na Wataalamu wa Afya.

“Nakuombeni wananchi tuendelee kuchukua tahadhari kwani maradhi haya yapo Zanzibar” Aliesema Mhe. Hemed

Aidha, Makamu wa Pili wa Rais aliwakumbusha wananchi kuendelea kuimarisha Umoja, Mshikamano na Upendo miongoni mwao ili kuwaunga mkono Viongozi wakuu wa Nchi kwa lengo la kufanikisha azma ya kuwafikishia maendeleo wananchi wake.

Alifafanua kuwa, kitendo cha kuendeleza ushirikiano kinapelekea kumisha Amani Nchini jambo ambalo zipo baadhi ya Nchi zimeikosa tunu hiyo na kushindwa kutekeleza mambo ya msingi ikiwemo Ibada na shughuli nyengine za kijamii.

Nae, Khatib wa sala ya Ijumaa Sheikh Salum Rashid aliwasisitiza waumini kuendelea kushikamana na suala la ibada ili kufikia daraja ya uchamungu na kupata radhi kutoka kwa Allah (S.W).

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.