Habari za Punde

Makala Kumbukizi ya Miaka 22 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere · Sababu za Kumuenzi Tunazo

Na: Lillian Shirima – MAELEZO

Oktoba 14, kila mwaka ni siku ambayo Taifa linaadhimisha kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa letu  na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwalimu Nyerere  alifariki  dunia Oktoba 14, 1999 katika Hospitali ya Mt. Thomas iliyopo London, Uingereza alipokuwa  akipatiwa matibabu na kuacha simanzi kubwa ndani na nje ya nchi.

Mzee Michael Ndesamburo (82) Mkazi wa Kimara mwisho Jijini Dar es Salaam anasema kwamba sababu kubwa ya kuenzi mchango wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zinatokana na maono na matendo yake  juu ya taifa la watanzania ambayo ni msingi wa  amani, heshima na utu mwanadamu hadi hii leo.

‘Mwalimu Nyerere anakumbukwa na kuheshimiwa ndani na nje ya mipaka yaTanzania si kwasababu alikuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, hata kidogo, alikuwa  kiongozi aliyepigania umoja na utu wa mwanadamu hata kufanikiwa kujenga taifa lenye amani’. Amesema Mzee Ndesamburo.

Aidha, amesema Mwalimu Nyerere alikuwa nguzo imara  iliyounganisha taifa la Tanganyika (wakati ule), ambapo alitumia busara kuliongoza hadi kupata uhuru mwaka 1961 bila kumwaga damu kama mataifa mengine hatuna budi kuenzi mchango wake.

Akielezea hali ilivyokuwa wakati wa ukoloni, Mzee Ndesamburo  amesema, wakati wa ukoloni watu hawakuishi kwa kushirikiana bali waliishi kama taifa la mkusanyiko wa watu waliodharauliwa na kunyanyaswa na utawala wa Mwingereza. Maisha ya jamii yalighubikwa na mifadhaiko ya utengano pamoja na umasikini.

Wajerumani walianza kututawala mwaka 1884 hadi 1918 wakifuatiwa na Waingereza mwaka 1918 hadi taifa huru la watu wa Tanganyika lilipoundwa, baada ya kutawaliwa na wakoloni kwa miaka  takriban 77.

‘Ilikuwa ni mahangaiko na manyanyaso, tulifanya kazi kwenye mashamba ya kahawa  kwa ujira mdogo  sana, hatukupata faida yoyote sasa hivi mambo yamekuwa ya kisasa…”. Ameendelea kufafanua Mzee Ndesamburo.

Mzee Ndesamburo alifika Jijini Dar es Salaam akitokea Tarakea katika Mkoa wa Kilimanjaro mwanzoni mwa miaka ya 70 akijishughulisha na ushonaji wa viatu na wakati mwingine akitengeneza saa za mkononi zilizoharibika kwenye eneo la Posta, (maarufu Posta ya Zamani).

Anasema, akiwa katika eneo hilo la Posta mara kadhaa anasema alishuhudia msafara wa Mwalimu Nyerere ukipita katika barabara ya Sokoine (Sokoine Drive) ukitoka au kuelekea Ikulu na taratibu alijenga mazoea ya kusimama kando  barabara hiyo  ambapo Mwalimu alikuwa akiwapungia mkono.

 “Nakumbuka nilipata shauku ya kukimbilia barabara na kumpungia mkono akitoka ikulu, nilijisikia furaha sana kumwona”.

Amemtaja Mwalimu kama kiongozi aliyeishi maisha ya kawaida, mwadilifu na mzalendo, aliyetamani kuona watu wakiishi pamoja na kushirikiana katika shughuli za kimaendeleo.

Licha ya wingi wa makabila tuliyonayo nchini, Mwalimu  Nyerere atakumbukwa kwa namna alivyoweza kuwaunganisha watanzania katika lugha moja ya kiswahili iliyoleta  maelewano,  kutambuana na kuishi kama ndugu hali iliyoleta  ustawi wa amani na umoja wa taifa letu hadi hii leo.

Akizungumzia kuhusu Muungano amesema, Mwalimu alipenda kuona watu wakiishi kwa amani hivyo kwa kushirikiana na Mwanamapinduzi Shupavu, Mzee Abeid Amani Karume aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, waliunganisha Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 26, 1964

‘Sina wasiwasi tutasheherekea miaka 58 ya Muungano tukiwa na mshikamano imara zaidi ifikapo Aprili, 2022, sherehe zitafanyika ndani ya taifa salama na utulivu kutokana na jitihada ziliyofanywa na Mwalimu ambazo viongozi wetu wa awamu zinaziendeleza”. Anasema Mzee Ndesamburo.

Misingi ya umoja na mshikamano iliyowekwa na Wazee wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume imeendelewa kuimarishwa na viongozi wa awamu zote zilizofuatia kwa upande wa Muungano na Zanzibar na kusababisha utulivu nchini.

Tunamuenzi Mwalimu kwa utayari wake wa kusaidia mataifa mengine ya Afrika kupata uhuru. Mwalimu hakuwa mbinafsi, alihimiza watu kuheshimiana bila kujali rika, dini, kipato, kabila au rangi akiamini kuwa binaadamu wote ni sawa.

Alikuwa mtetezi wa amani, mlinzi wa rasilimali za taifa, aliyechukizwa na ukabila, udini, ubadhirifu wa mali ya umma, ulafi wa madaraka , rushwa na uzembe ulioanza kujitokeza katika ukusanyaji wa kodi.

Katika hotuba zake hakuacha kukemea dosari zilizojitokeza  wakati wa utawala wake na hata baada ya kung’atuka  madarakani. Alisisitiza ukusanywaji wa kodi kwa maendeleo ya taifa.

Mathalani; katika hotuma yake ya Maadhimisho ya  Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) iliyofanyika Jijini Mbeya Mwaka 1995, Mwalimu  pamoja na mambo mengine alikemea  athari za kutokukusanywa kodi ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi..

 ‘…hamkusanyi kodi kwanini? Kwasababu kutokukusanya kodi mnaviua viwanda vyetu nyumbani hapa…..hata kisingizio cha kusema ni IMF, ni World Bank si kweli, baadhi yao  hao IMF na World Bank ndio wanasema kusanyeni kodi….kwanini hamkusanyi kodi’. Alisema Mwalimu Nyerere.

Kwa kuzingatia umuhimu ya ukusanyaji kodi kwa maendeleo ya taifa, Julai, 2020 Tanzania  imefanikiwa kuingia kwenye kundi la nchi za uchumi wa kati ambapo pato la kila Mtanzania limeongezeka hadi kufikia dola za kimarekani 1,080, ikiwa ni zaidi ya kigezo cha dola za kimarekani 1,036 cha kuingia kundi hilo. 

Mafanikio haya yamechangizwa na utulivu wa kisiasa, amani na mshikamano katika jamii hali iliyoruhusu Serikali kuelekeza nguvu kubwa katika kusimamia ukuzaji wa uchumi.

Zimepita awamu nne (4) tangu Mwalimu Nyerere (Baba wa Taifa) alipong’atuka kwa hiari madarakani mwaka 1985 na kurudi kijijini kwake Butiama hadi umauti ulipomkuta.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliingia madarakani rasmi Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Pombe Magufuli tarehe 17 Machi, 2021.

Katika hotuba yake ya kwanza aliyoitoa Bungeni Mjini Dodoma Aprili, 2021, Mhe. Samia  Suluhu Hassan alisema Serikali yake itaendelea kudumisha mazuri ya awamu zilizopita ikiwa ni pamoja na kulinda tunu za taifa ambazo ni amani, umoja na mshikamano wa watanzania. TAFUTA NUKUU

“Jambo la kwanza muhimu kabisa tutakalolipa kipaumbele ni kuendelea kulinda na kudumisha tunu za taifa letu, yaani  amani, umoja na mshikamano…….”.  Alisema Rais Samia Suluhu Hassan”.

Licha ya kuendelea kudumisha mshikamano na umoja wa kitaifa, tunaadhimisha miaka 22 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere  huku Serikali ikiendelea na juhudi za kuhakikisha maendnchi inazidi kusonga mbele kiuchumi na kijamii.

Moja ya mikakati wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliyoahidi ni kuimarisha  mazingira bora ya uwekezaji nchini yatakayovutia uwekezaji zaidi pamoja na ukusanyaji kodi ya Serikali.

Kwa kipindi kifupi toka aingie madarakani, miradi ya uwekezaji imeongezeka na kufikia dola  bilioni 3.5 mwaka huu ukilinganisha na dola milioni 647 katika kipindi cha mwaja jana.

Mbali na mafanikio hayo. taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO ambaye ni  Msemaji wa Serikali Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa  Oktoba 2, 2021, ilionesha ukusanyaji wa mapato kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) umeongezeka ikilinganishwa na mwaka 2020 ambapo zilikusanywa Shilingi Trilioni 1 na Bilioni 703 sawa na asilimia 80 ya malengo ya kukusanya Shilingi Trilioni 2 na Bilioni 229.

Makusanyo ya mwezi Septemba, 2021 ni Shilingi Trilioni 1 na Bilioni 970 sawa na asilimia 93 ya malengo ya kukusanya Shilingi Trilioni 2 na Bilioni 128.

Serikali ya Awamu ya Sita imeongeza kasi  kuhakikisha miradi yote ya kimkakati iliyoanzishwa kama vile Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme Mto Rufiji (JNHPP), Reli ya Kisasa (SGR), Barabara na mingine mingi inakamilika kama ilivyopangwa kwakuwa lengo ni kuleta maendeleo kwa wananchi.

Tuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere Kiongozi aliyekuwa na juhudi za kutimiza ndoto za watanzania akiamini kwamba tunu za umoja na amani tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu ni msingi wa malezi ya taifa huru katika kuleta maendeleo ya watu wake.

Pumzika kwa amani, Hayati Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Tanzania ipo imara.

MWISHO.

Kwa upande wa huduma ya afya kazi kubwa iliyofanywa tangu 2015 mpaka sasa. Tumefanikiwa kuongeza idadi ya hospitali kutoka ..zilizokuwapo wakati tunapata uhuru hadi kufikia hospitali ……hivi sasa. Zahanati nazo zimeongezeka kutoka …..mwaka 1961 hadi 4,679 hivi leo. Tumeongeza pia idadi ya vituo vya afya vijijini kutoka vituo 22 tulivyorithi kutoka kwa wakoloni hadi vituo 481 vya sasa. Watu wengi zaidi sasa wanapata huduma ya afya kuliko ilivyokuwa wakati wa ukoloni. Afya za Watanzania wengi zimeimarika zaidi sasa kuliko ilivyokuwa. Watu sasa wanaishi miaka mingi zaidi na ndiyo maana idadi ya watu ni mara….ya wale waliokuwepo wakati nchi yetu inapata uhuru.

 Bado tunayo kazi kubwa ya kuboresha huduma ya afya nchini kwa kujenga zahanati na vituo vya afya na hospitali zaidi. Kuboresha huduma ya watoto na mama wajawazito na kupambana na maradhi yanayoua watu wengi kama vile malaria, ukimwi, kifua kikuu na mengineyo.

Tangu tupate uhuru Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kupanua huduma za usafiri wa barabara, reli, anga na usafiri wa majini. Tumepata mafanikio makubwa na ya kutia moyo. Maeneo mengi vijijini sasa yanafikika kwa barabara.

Bila miundombinu bora uchumi wetu hauwezi kukua haraka. Pia panapokuwepo na barabara watu hutumia magari badala ya kutembea kwa miguu, hivyo kufanya maisha kuwa rahisi na bora zaidi.

Aidha, Serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri ya kiuchumi na kibiashara ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza zaidi nchini mwetu. Pia tutahakikisha kuwa vikwazo vinavyokwamisha uanzishaji na uendeshaji biashara hapa nchini vinaondolewa mapema ili kuimarisha sekta ya biashara na uwekezaji ambayo ni muhimu sana katika kuleta ajira nchiniSerikali itaendelea na kazi ya kukamilisha programu ya uwekezaji katika sekta utalii miundombinu ili kurahisisha mawasiliano na hivyo kuchochea kukua kwa shughuli za kiuchumi na kibiashara hapa nchini.

Reli ya TRC na TAZARA na viwanja vya ndege pamoja na kuviimarisha na kuboresha vilivyopo

kila mmoja wetu afanye kazi kwa bidii na maarifa ili kwa pamoja tusukume mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Jambo hili linawezekana ikiwa sote tutadhamiria hivyo. Tukumbuke msemo maarufu wa muasisi wa taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere usemao………………….

Kwa upande wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nayo tumepata mafanikio makubwa. Hali ya maisha ya Watanzania ilivyo leo sivyo ilivyokuwa wakati Mwalimu anang’tuka madarakani 1985

Wakati tunapata uhuru hali ya upatikanaji wa elimu nchini ilikuwa ni duni sana. Sehemu ndogo sana ya watu wetu waliweza kupata elimu. Hivyo, watu wengi walikuwa wanakabiliwa na tatizo la ujinga.

Mwalimu Nyerere aliutangaza ujinga kuwa moja ya maadui watatu wa nchi yetu pamoja na umaskini na maradhi. Hali ilikuwa hivyo kwa sababu ya ufinyu wa fursa za kupata elimu hasa kwa Waafrika. Kwa sababu ya ubaguzi Serikali ya ukoloni haikujali na hivyo haikujihusisha vya kutosha na elimu kwa wananchi.

Kazi hiyo iliachiwa mamlaka za wenyeji na mashirika ya dini na hasa makanisa kuifanya pale ambapo yalipobahatika kuwepo. Hata pale Serikali ilipojihusisha ilijali zaidi elimu ya kupata makarani tu na siyo kupata watu wenye taaluma muhimu kwa maendeleo kama vile udaktari, uhandisi na kadhalika. Kwa jumla, wakoloni walikuwa na sera ya makusudi ya kutokuwasomesha Waswahili ili wawatawale vizuri.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.