Habari za Punde

Ziara ya Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Wilayani Lindi leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya shilingi 100,000/=  Rukia Said ambeye ni dereva wa mtambo maalum unaotumika  katika ujenzi wa barabara (roller) wa Kampuni ya  CHIBESHI Construction Company Limited , baada ya Waziri Mkuu kuvutiwa na kazi nzuri iliyofanywa na kampuni inayojenga barabara ya Hingawali hadi Navanga yenye urefu wa Kilomita 14.1 na barabara ya Navanga hadi Pangabohi yenge urefu wa kilomita 8 katika Jimbo la Mtama, Oktoba 5, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya Mtama Mkoani  Lindi,akiwa katika ziara yake Mkoani humo.

Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza  nao pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi kwenye viwanja vya Halmashauri hiyo,  Oktoba 5, 2021.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.