Habari za Punde

Katibu Mkuu wa CCM Chongolo Aendelea na Ziara Yake

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akimkabidhi cheti kijana Revely Reonady wa Kambi ya Vijana wa kujitolea katika ujenzi wa shule ya Sekondari Bukama Kata ya Kagoma kama ishara ya kutambua mchango wao katika shughuli za kimaendeleo ambapo vijana zaidi ya 90 wa wilaya ya Muleba huweka kambi na kujitolea katika kazi za kimaendeleo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Ndugu Elias Kayandabila mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya Sekondari Bukama Kata ya Kagoma ambapo vijana zaidi ya 90 wa wilaya ya Muleba wameweka kambi na kujitolea katika kazi za kimaendeleo. (Picha na CCM Makao Makuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.