Habari za Punde

Ligi Kuu Zanzibar: Malindi yaitambia Black Sailor yaibuka na ushindi wa 1-0

 Na Mwajuma Juma

MABAHARIA wa timu ya soka ya Malindi wamewatambia Black Sailor kwa kuifunga bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliochezwa uwanja wa Mao Zedong.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani wa sina yake ulichezwa majira ya saa 10:00 za jioni ambapo Malindi walipata bao lao hilo dakika ya 18 kupitia kwa Said Salum Abeid.

Katika mchezo huo Malindi walicheza wakiwa pungufu baada ya mwamuzi Ramadhan Kesi kumtoa kwa  kadi nyekundu mchezaji wao Humud Suleiman Abdalla dakika ya 54.

kwa matokeo hayo Malindi imefikisha pointi 17 na kuwa nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na KMKM wenye pointi sawa wakiwa mbele kwa idadi ya mabao ya kushinda na kufungwa.

Aidha katika  uwanja wa Amaan maafande wa JKU walitoka sare tasa na  Kipanga  wakati mabingwa watetezi wa ligi hiyo KMKM ambao ndio vinara wa msimamo wa ligi hiyo wakatoka sare kama hiyo na Yoso Boys walipocheza Gombani.

Hata hivyo uwanjani hapo Gombani wakati wa saa 10:00 za jioni Taifa ya Jang'ombe iliifunga Selem View mabao 2-0, ushindi ambao umewafikisha pointi 14 na kuwa nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.