Habari za Punde

Maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaanza kwa Bonanaza la Afya kisiwani Pemba

AFISA Mdhamini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ Thabit Othman Abdalla, akipima sukari na Dr Omar Khatib, wakati wa bonanza la Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, boanza lililofanyika Gombani Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

DR.Mohamed Farouk akimpima Presha Afya Ali Said Ali mmoja wa wananchi waliohudhuria bonanza la Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, boanza lililofanyika Gombani Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Dr.Mtumwa Salum Suleiman kutoka kituo cha Afya Gombani, akimchoma akimchanja chanjo ya UVIKO 19 Hamisa Omar Hamad, wakati wa bonanza la Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, boanza lililofanyika Gombani Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WASANII kutoka kikundi cha Mwinyi Mpeku cha Wete wakitoa moja ya igizo lao, katika bonanza la Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, bonanza lililofanyika Mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)

MCHEZAJI wa Timu ya Chake Chake Star Najati akiruka juu na kufunga goli(kikapu), wakati wa boanza la Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, bonanza lililofanyika Mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)


AFISA Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Salum Ubwa Nassor, akimkabidhi seti ya Jezi na bahasha ya Fedha Taslimu Kepteni wa Timu ya Mkoroshoni Ali Seif Ali, baada ya kuibuka na mshindi wa kwanza kwa kuichapa Younger Islander bao 2-0.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.