Habari za Punde

Naibu Waziri Maliasi na Utalii Mhe.Mary Masanja Amekutana na Kuzungumza na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amekutana na watendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda kwa lengo la kujifunza uwekezaji kwenye Utalii wa Mikutano katika kikao kilichofanyika Kigali- Rwanda.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga (kulia) akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) na watendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda kuhusu uwekezaji kwenye utalii wa mikutano kilichofanyika katika ofisi za bodi hiyo Kigali nchini Rwanda.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utalii,Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Utalii, Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Emmanuel Nsabimana mara baada ya kikao cha kujifunza uwekezaji kwenye Utalii wa Mikutano kilichofanyika katika ofisi za Bodi ya Maendeleo ya Rwanda Kigali nchini Rwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Ariella Kageruka mara baada ya kikao cha kujadili uwekezaji kwenye Utalii wa Mikutano kilichofanyika katika ofisi za Bodi ya Maendeleo ya Rwanda Kigali nchini Rwanda.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati) katika picha ya pamoja na watendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda mara baada ya kikao cha kujifunza uwekezaji kwenye Utalii wa Mikutano kilichofanyika katika ofisi za Bodi ya Maendeleo ya Rwanda Kigali nchini Rwanda.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) leo amekutana na watendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda kwa lengo la kujifunza kuhusu uwekezaji katika Utalii wa Mikutano.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Bodi ya Mikutano ya Rwanda ,Kigali.

Amesema kuwa Bodi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuvutia watalii wa mikutano kwa kushirikiana kwa karibu na Sekta Binafsi.

“Kwa mfano kuna ukumbi mkubwa wa mikutano unaomilikiwa na Serikali unaendeshwa na Sekta Binafsi na umefanikiwa kuvutia watalii wengi” ameongeza Mhe. Masanja.

Amesema kupitia ujuzi uliopatikana katika kikao hicho, Tanzania itaenda kuutumia ili kutangaza na kuvutia watalii wa mikutano kutoka ndani na nje ya nchi na hatimaye kuikuza Sekta ya Utalii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.