Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi afanya ziara ya ghafla kutembelea visima vya Maji Safi na Salama Bumbwisudi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji,Nishati na Madini Mhe.Suleiman Masoud Makame (katikati)  pamoja na watendaji wengine wakati alipofanya ziara ya Ghafla kwa kutembelea visima vya Maji Safi na Salama Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa Mjini Magharibi leo.[Picha na Ikulu] 25/11/2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisisitiza jambo kwa watendaji wakati alipofanya ziara ya Ghafla kwa kutembelea visima vya Maji Safi na Salama Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa Mjini Magharibi leo (katikati) Waziri wa Maji,Nishati na Madini Mhe.Suleiman Masoud Makame,(wa tatu kulia) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi"A" Mhe.Suzan Peter Kunambi.[Picha na Ikulu] 25/11/2021
Mlinzi katika Visima vya Maji Safi na Salama (ZAWA) Bw.Hussein Ismail akitoa changamoto zinazowakabili katika kazi zao wakati  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipofika maeneo  ya Visima vya Maji Safi na salama (ZAWA)Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi"A" Mkoa wa Mjini Magharibi kuangalia tatizo lililopelekea kukosekana kwa huduma hiyo.[Picha na Ikulu] 25/11/2021.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia) akizungumza na Wananchi wanaoishi karibu na  maeneo  ya Visima vya Maji Safi na Salama (ZAWA)Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi"A" Mkoa wa Mjini Magharibi wakati alipofanya ziara ya ghafla leo kuangalia tatizo lililopelekea kukosekana kwa huduma hiyo (kulia)Waziri wa Maji,Nishati na Madini Mhe.Suleiman Masoud Makame,(wa pili kushoto) Dkt.Mngereza Mzee Miraji).[Picha na Ikulu] 25/11/2021.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.