RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa
Mufti. Sheikh.Khalid Ali Mfaume, na (kulia kwa Rais) Mtoto wa Marehemu na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, wakiitikia dua baada
ya kumalizika kwa Sala ya Jeneza kuusalia mwili wa Baba Mzazi wa Mjane wa
Maalim Seif Sharif Hamad, Mama Awena Sanani Masoud,iliofanyika katika Msikiti
wa Masingini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 22-11-2021, na (kushoto kwa
Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwafariji Watoto wa Marehemu Sanani
Masoud, baada ya kumalizika kwa Sala ya Jeneza iliofanyika katika Msikiti wa
Masingini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 22-11-2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutowa mkono wa pole kwa
Mjane wa Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.Mama Awena Sanani na familia yake, alipofika nyumbani kwa marehemu masingini Wilaya ya Magharibi”A” Unguja kutowa
mkono wa pole kwa familia leo 22-11-2021.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kumuombea Baba Mzazi wa Mjane wa Maalim Seif Sharif Hamad Mama Awena Sanani Masoud, alipofika nyumbani kwa marehemu kutowa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu leo 22-11-2021.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment