Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiunduzi Mhe.Dk,.Hussein Ali Mwinyi Ameweka Jiwe la Msingi Hoteli za Kitalii za Riu Jambo Nungwi na Emerald Zanzibar Resort and SPA Matemwe.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Nungwi wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Mradi wa Ujenzi wa  Hoteli ya Kitalii ya Riu Hotels &Resots Nungwi. Ikiwa ni shamrashamra za mwaka mmoja wa Uongozi wake.(Picha na Ikulu) 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza haja kwa wawekezaji kuhakikisha miradi wanayoitekeleza inawafaidisha wananchi wanaoishi karibu na miradi hiyo.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati akiweka mawe ya msingi  katika ujenzi wa Hoteli mpya ya kisasa ya Riu Jambo iliyopo Nungwi pamoja na Hoteli ya Emerald Zanzibar Resort and SPA iliyopo Matemwe Mbuyuni Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kutimiza mwaka mmoja tokea aingie madarakani hapo Novemba mwaka jana Novemba 2020.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi ambaye alifuatana na Mama Mariam Mwinyi alisisitiza kwamba ni vyema miradi inayotekelzwa iwe inawafaidisha wananchi kwa kuweza kupata ajira sambamba na kuweza kuuza bidhaa zao.

Alieleza kwamba ni vyema uongozi wa Mkoa na Wilaya ukaja kuweka utaratibu maalum wa kuhakikisha bidhaa zao wanaziuza katika Hoteli hizo kwenye maeneo hayo badala ya kuhangaika kutafuta masoko.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba ni vyema wawekezaji wa miradi hiyo wakaelewa changamoto zinazoikabili jamii katika maeneo yenye miradi yao ili wakaweza kuwasaidia hasa katika miradi ya elimu, afya, maji na mengineyo kwa kushirikiana na Serikali.

Rais Dk. Miwnyi alisema kuwa ni vyema vijana wakafaidika na kazi ama ajira katika miradi hiyo zikiwemo Hoteli hizo za kisasa na kusisitiza kwamba kuna kila sababu ya vijana katika maeneo hayo kuongeza ujuzi kwa kupata elimu inayokwenda na miradi hiyo hasa ikizingatiwa kwmaba vyuo vya kutoa elemu hiyo vipo hapa hapa Zanzibar kikiwemo Chuo cha Utalii Maruhubi.

Rai Dk. Mwinyi akiwa Matemwe Mbuyuni mara baada ya kuweka jiwe la msingi akiwasalimia wananchi alieleza kwamba utalii ndio sekta muhimu inayoimarisha pato la Taifa huku akisisitiza kwamba .

Rais Dk. Miwnyi aliwasisitiza vijana kUwa tayari kufanya kazi “Tuwe tayari kufanya kazi...kwani kuna vijana wengi hawajawa tayari kufanya kazi, hivyo ni vyema wakawa tayari na sisiSerikali iko tayari kufanya kazi kwa mashirikianio ya pamoja”,alisema Dk. Mwinyi.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Mwinyi aliwapongeza wakandarasi wa ujenzi wa Hotelihizokutokana na kasikubwa ya ujenzi wanayokwenda nayo ambayo inakwenda sambamba na kasi ya Awamu ya Nane.

Nao wawekezaji wa Hoteli ya Riu Jambo ambapo ujenzi wake ulianza Januarimwaka huu 2021 waliwahakikishia wavuvi wa maeneo hayo kwamba mradi wa Hoteli yao utakapokuwa tayari kufanya kazi samaki wote watakaovuliwa katika eneo hilo watanunuliwa na hoteli yao ili kuhakikisha wavuvi hao wanapata soko la uhakika pamoja na kuwajengea soko na miradi mengine ya jamii.

Kwa mujibu  wa maelezo ya uongozi wa Hoteli hiyo, mradi huo unatarajiwa ujenzi wake kumaliza mnamo Septemba mwakani 2022, na utaajiri  wafanyakazi 400 huku hoteli hiyo itakuwa na vyumba 468 ambapo ujenzi wake utagharibu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 70.

Kwa upande wa Hoteli ya Emerald Zanzibar Resort and SPA ambayo ujenzi wake ulianza Novemba mwaka jana 2020 unatarajiwa kumaliza mwakani 2022, mradi ambao kwa akuanzia utakuwa na vyumba 250 na hadi kumaliza katika awamu zijazoitakwua na vyumba 1000.

Kitengo cha Habari

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.