Habari za Punde

Wakandarasi wa Makampuni ya Ujenzi Watakiwa Kujitathimini Namna ya Kutekeleza Miradi.

Na Maulid Yussuf WEMA ZANZIBAR

Wakandarasi kutoka makampuni mbalimbali ya ujenzi, wametakiwa kujitathmini namna gani wataweza kutekekeleza mradi wa mapambano dhidi ya janga la UVIKO 19 katika Elimu.

Akizungumza na Wakandarasi hao wakati wa Mkutano wa kuwapa uelewa wa mradi huo, katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Mjini Unguja, Mkurugenzi Idara ya Mipango Sera na Utafiti, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali bw Khalid Masoud Waziri amesema mradi huo tayari umeshaanza kutekelezwa tokea mwezi wa October na unatarajiwa kumalizika mwezi wa Juni mwakani.

Bwana Khalid amefahamisha  kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa Skuli 35 za Maandalizi, Msingi na Sekondari kwa Unguja na Pemba ambpo kila Wilaya zitajengwa Skuli mbili za maandalizi zenye madarasa manne au matano.

Pia amesema mrasi huo uthusisha ujenzi wa Vyoo 1693 pamoja na kufanyiwa matengenezo makubwa Skuli 22 pamoja na kujengwa nyumba za walimu 10 katika visiwa vitano vya Zanzibar.

Aidha Mkurugenzi Khalid ametumia nafasi hiyo kuwapa Wakandarasi hao salamu za Mhe Waziri wa Wizara hiyo kuwa amewataka kujidhatiti wao wenyewe kwa asilimia mia moja katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo pamoja na kuwa waaminifu, ili Serikali iendelee kuwa na imani nao katika kuwapa miradi mengine.

Aidha amewataka kuhakikisha wanapotekeleza mradi huo kuzingatia muda na ubora wa  viwango kutokana na bidhaa watakazozitumia ili kuepuka hasara inayoweza kuwakuta hapo baadae.

Hata hivyo Mkurugenzi Khalid amewataka kujifikiaria huku wakitambua kuwa saini za makubliano ya ujenzi zitafanyika  mwezi wa Disemba, na kuwatoa khofu juu ya malipo yao  kuwa Wizara itawapatia kwa mujibu  watakavyokubaliana.

Nao baadhi ya Wakandarasi wa kampuni mbali mbalimbali wameiomba Wizara kuwawekea uwazi juu ya mgao PACKAGE wa mradi huo utakavyokuwa ili kuweza kujitathmini vizuri pamoja na kuepuka kuomba PACKAGE moja kwa wakandarasi wa kampuni tofauti.

Aidha wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwaamini wakandarasi wazalendo kwa kuamua kuwapa mradi huo mkubwa, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali yao katika kuleta maendeleo nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.