Habari za Punde

Walimu wa Madrasa Watakiwa Kutumia Fursa Waliyanayo Kulea Watoto Katika Maadili Mazuri.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akitoa nasaha zake katika hafla ya maulid yaliyoandaliwa na madrasatu swifatu nabawiyyatil karima
    Waumini wa dini ya kiislamu waliohudhuria katika    maulid yaliyoandaliwa na madrasatu swifatu nabawiyyatil karima

Na. Kassim Abdi.OMPR.

Walimu wa Madrasa nchini wametakiwa kutumia fursa walionayo katika kulea watoto ili kuwa maadili mema.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo katika hafla ya Maulid iliyoandaliwa na Madrasatu Swifatu Nabawiyyatil Karima (kwa msolopa) Kilimani Jijini Zanzibar.

Amesema juhudi za walimu wa madrasa hiyo ni jambo la kupongezwa, akitolea mfano kuzalisha watu wenye uwezo wa taaluma tofauti ambao hutumia taaluma zao katika kuiletea maendeleo Zanzibar,  na kuzitaka madrasa nyengine kuiga mfano huo.

Amesema iwapo walimu wa Madrasa watashirikiana kwa pamoja kwa kuwakuza wanafunzi katika malezi mema Zanzibar itapelekea kupata wataalamu wenye maadili, ambapo wataweza kuwajibika kwa kuzingatia malezi walionayo.

Mhe. Hemed amewataka waumin hao kujijenga na tabia njema kwa kufuata maelekezo na muongozo wa Mtume Muhammad (S.A.W) katika suala la kufanya Ibada, ili kufikia darja ya kuwa wachamungu ikiwa ndio lengo la kuletwa Duniani.

Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar ametumia fursa hiyo kuwataka walimu wa Madrasa kuzidisha juhudi ya kutoa elimu bora, ili jamii kuweza kumjua mola wao na kumuabudu kama ilivyoeleza sheria.

Akitoa khutba katika hafla hiyo Ustadh Othman Pocho kutoka Masjid Shadhuly Dar -es- Salaam amewataka waumini hao kumfuata Mtume Muhammad (S.A.W)   ikiwa ndio kigezo chema kwa waumini wa dini ya kiislamu, na kuwataka kujijenga na tabia ya kusameheana.

Madasatu Swifatu Nabawiyyatil Karima ( Kwa msolopa) ya kilima I imeanzishwa mwaka 1975 kwa sasa ina miaka 46 tokea kuasisiwa kwake  ambapo kila mwaka huandaa maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.