Habari za Punde

Wizara ya Maliasili na Utalii Yafanikiwa Kutegua Mitego 380 ya Kuulia Wanyamapori Katika Hifadhi ya Nyerere.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro  akiwa amefungwa mguu kwa kutumia nyaya ya umeme na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess ikiwa ni mfano jinsi wanyamapori wanavyonaswa katika mitego ambayo imekuwa ikitegwa na majangili kwa ajili  ya kuuwa wanyamapori  kwa ajili ya kujipatia kitoweo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro  akizungumza na  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa kikosi maalum cha kutegua mitego ilitegwa katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Wengine ni baadhi ya ujumbe kutoka Balozi wa Ujerumani nchin  Tanzania pamoja na Watumishi wa Hifadhi ya Nyerere.

Wizara ya Maliasili na Utalii  imefanikiwa kutegua nyaya za umeme 380 zilizokuwa zimetegwa katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ikiwa ni aina mpya ya ujangili wa wanyamapori kwa ajili ya kitoweo

Akizungumza  hivi karibuni, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro  akiwa ameambatana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess  katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere iliyopo mkoani Morogoro ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kufadhili mradi huo wa kunasua mitego iliyotegwa kwa ajili ya kuuwa wanyamapori katika Hifadhi hiyo

Amesema  Majangili  hao wamekuja na mbinu mpya mara baada ya Serikali kupambana na ujangili wa Biashara ya wanyamapori wakubwa kama vile tembo pamoja na faru

Dkt. Damas Ndumbaro amesema ujangili wa wanyamapori kwa ajili ya kitoweo kwa kutumia nyaya za umeme umeanza kuchukua sura mpya   huku Serikali ikiahidi kuendelea kupambana na mbinu  hiyo mpya

Dkt. Ndumbaro amesema tokea kikosi maalumu kilichoundwa kwa kushirikiana na wanavijiji kwa ajili ya kutegua mitego hiyo jumla ya wanyamapori watatu walikutwa wamekufa mara baada ya kunaswa kwenye mitego hiyo

Ametaja wanyamapori hao waliokutwa wamekufa kuwa ni twiga moja pamoja na swala wawili hata hivyo Dkt. Ndumbaro amesema kupitia mradi huo wa kunasua mitego Wizara hiyo imekuja na mbinu ya kuwashirikisha wanavijiji wanaopakana na Hifadhi kwa ajili kupambana na majangili hao.

Akizungumzia aina mpya hiyo ya ujangili, Dkt. Ndumbaro amesema majangili hao wamekuwa wakitega mitego hiyo kwa ajili ya kuwanasa wanyapori kwa ajiili ya kujipatia nyama ya kula

Dkt. Ndumbaro amesema licha ya mitego hiyo kutegwa ajili ya kuuwa wanyamapori wadogo wadogo kwa ajili ya kitoweo lakini mitego hiyo inaweza kunasa hata wanyamapori wakubwa kama vile tembo wanyamapori wengine wakubwa 

Amefafanua kuwa baadhi ya Jamii  zimekuwa zikiendeleza imani potofu ya kula nyamapori kwa kuamini kuwa ndo nyama bora kupita zote kuwa  hali imekuwa ikichangia ujangili kwa ajili ya kitoweo.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mhe. Regine Hess amesema Serikali yake iliamua kufadhili mradi wa kutegua mitego hiyo baada ya Serikali ya Tanzania kufanikisha kukomesha ujangili kwa asilimia 90 hususan ujangili wa biashara.

Mhe. Hess ameleezea kuwa mradi huo pia umeonesha mafanikio makubwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo mitego mingi imeweza kuteguliwa.

Aidha, Balozi huyo ameipongeza Serikali ya Tanzania kuwa Serikali ya kwanza Barani Afrika kwa  kusimamia shughuli za uhifadhi kiukamilifu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.