Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe
la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT
II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa katika sherehe
zilizofanyika Mbagala Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021. Wa
kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Wengine katika
picha ni Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel
Chongolo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila wakati akitoa maelezo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa kabla ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mradi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbagala hawaonekani pichani mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa zilizofanyika Mbagala mkoani Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment