Habari za Punde

Kongamano la vijana la kuadhimisha siku 16 za harakati za kupinga Ukatili na udhalilishaji wa kijinsia laendelea
 Ni harakati za siku 16 za kupinga ukatili WA kijinsia. Tumekuwa na wakati mzuri sana chini ya shirika la SOS ambapo Wanafunzi wa kike kutoka sehemu mbalimbali walialikwa.

Wasichana wametoa maoni yao na pia kuelezea vikwazo vinavyosababisha wao kushindwa kufanya vyema Darasani. Sababu mojawapo ikiwa ni kutopata muda wa kutosha kujisomea, Waalimu kutotoa hamasa ya kuwatia Moyo na pia kutakiwa kimapenzi.
Wasichana kutoka kisiwa cha Tumbatu wanakabili wakati mgumu wa Waalimu wa somo la Sayansi kadhalika Waalimu wa masomo ya ziada.
Vilevile hawafikiwi kwa urahisi au kujumuika katika masuala yanayowagusa ikilinganishwa na Wasichana wa maeneo mengine ya kisiwa cha Unguja
Kisiwa cha Tumbatu ni Kisiwa cha pekee kisichokuwa na Gari na pia huwezi kufika mahali hapo kwa njia yoyote isipokuwa kwa kutumia Boti.
Wasichana wote kwa ujumla wameonyesha ari ya kuwa Nyota kwenye jamii ya mabadikiko katika kuelekea kwenye Tanzania na Visiwa vya Zanzibar kutokuwa na matukio ya kikatili.
Watoa mada katika maadhimisho hayo ni Asasi ya kiraia Girl Gude na Mbunge kutoka viti maalum kusini Pemba Bi Munira Mustapha Khatib.
UJUMBE WA MWAKA HUU NI
๐Ÿ‘‡
"Ipambe Dunia maliza ukatili dhidi ya Wanawake sasa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.