Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Tumbe Pemba Mhe.Amour Khamis Ametimiza Ahadi Yake Kwa Wananchi wa Tumbe.

Mbunge wa Jimbo la Tumbe Pemba Mhe,Amour Khamis Mbarouk akizungumza na Wananchi wa Jimbo lake wakati wa kukabidhi mipira ya kusambaza maji safi na salama kwa Wananchi wa Jimbo lake, kuondosha tatizo la maji katika shehia zote zilioko katika jimbo hilo, (kulia kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Salama Mbarouk.

Ugawaji wa vifaa hivyo uliofanyika katika shehia ya mihogoni na Wananchi wa Jimbo hilo wametowa shukuru kwa Mbunge wao kwa kuitekeleza vyema ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuwatatulia matatizo yao.

Na kutowa hongera kwa kuondoa  tatizo la maji la miaka 25 iliyopita nyuma tunalitatua kwa mwaka mmoja wa mbunge Mhe.Amour kutoka CCM.

Na.Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tumbe.Ndg.Hamad Juma Msoud.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.